...Msekwa kufikishwa mahakamani

...Msekwa kufikishwa mahakamani

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,967
Reaction score
166,365
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU), inakusudia kumfikisha mahakani aliyewahi kuwa spika wa bunge Mh. Msekwa kwa tuhuma za rushwa zinazohusiana na ufisadi wa kutisha katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Dr. Hoseah, asema wanakamilisha taratibu za kumfikisha mahakamani.

Hata hivyo, Msekwa mwenyewe ameonekana kushangazwa na hatua hiyo ya TAKUKURU.

Binafsi, ninachojiuliza ni kuwa DPP ataruhusu kweli kesi hiyo kufikishwa mahakamani? Ikumbukwe kuwa ofisi ya DPP imekuwa ikilalamikiwa na TAKUKURU kwa kuzuia kesi nyingi kufikishwa mahakamani kwa kisingizio kuwa ushahidi hautoshelezi kuwafungulia mashitaka wahusika.

CHANZO:JAMHURI
 
cc Anna Semamba Makinda na Job Ndugai
 
Aende tu ili mradi zisiwe ni siasa za kimtandao zenye lengo la kummaliza kisiasa.
 
Hivi Mama Anna Abdallah bado ni mkewe? Kama kweli ataitwa lini Anna Msekwa?
 
hahahaha uhuni tu kesi ya gendere jaji nyani unategemea nini hapo
 
Mtamuua huyu mzee kwa pressure!
 
DPP hataruhusu ili kukinusuru chama na fedheha zinazozalishwa na viongozi wake waandamizi.
 
Tunapigwa changa la macho hawa ni Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba !!!!!!!
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU), inakusudia kumfikisha mahakani aliyewahi kuwa spika wa bunge Mh. Msekwa kwa tuhuma za rushwa zinazohusiana na ufisadi wa kutisha katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Dr. Hoseah, asema wanakamilisha taratibu za kumfikisha mahakamani.

Hata hivyo, Msekwa mwenyewe ameonekana kushangazwa na hatua hiyo ya TAKUKURU.

Binafsi, ninachojiuliza ni kuwa DPP ataruhusu kweli kesi hiyo kufikishwa mahakamani? Ikumbukwe kuwa ofisi ya DPP imekuwa ikilalamikiwa na TAKUKURU kwa kuzuia kesi nyingi kufikishwa mahakamani kwa kisingizio kuwa ushahidi hautoshelezi kuwafungulia mashitaka wahusika.

CHANZO:JAMHURI
Naona wanataka kumpaka kinyesi asifae kwa matumizi ya binadamu kwa mwaka 2015. Kama anafaa anafaa tuu nakama hafai hafai tuu...Hizi ni mbimu za kupunguza nguvu za wagumbea Mjengoni kwa tiketi ya thithiemu.Wacha wafu wazikane.!!
 
Back
Top Bottom