Msekwa: CCM imepoteza sifa asili

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,035
Ameyasema hayo kwenye kitabu chake cha kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwa ccm. Amesema ccm imepoteza asili yake ya kutetea wanyonge

Chanzo: Magazeti ya leo

Wakati kesho CCM ikiadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa chama hicho, Pius Msekwa amechambua uwezo na udhaifu wake, akibainisha kuwa kimepoteza sifa ya asili ya kuwa chama cha wanyonge.

Msekwa amesema kuwa matukio mbalimbali yanayokikumba chama hicho, ikiwamo migogoro baina ya viongozi wake, makundi na tuhuma za ufisadi, yameathiri taswira yake kwa jamii.

Msekwa ambaye ni katibu mkuu wa kwanza wa Tanu na makamu mwenyekiti mstaafu (Bara), alibainisha kuwa CCM imepoteza sifa yake ya asili ya kuwa chama kinachojali wanyonge na kubebeshwa mzigo wa kuitwa “chama cha matajiri”.

“Migogoro miongoni mwa viongozi, hususan baina ya makundi yanayozozana au kuhasimiana ndani ya chama na tuhuma za ufisadi, imechangia kuifanya CCM ibebeshwe mzigo wa kuonekana kuwa ni chama kinachokumbatia mafisadi,” alisema.

Aliongeza kuwa CCM pia imeathiriwa na kujipenyeza kwa kasi kubwa kwa wafanyabiashara wasio waadilifu katika baadhi ya vikao vyake vya uamuzi.

Hata hivyo, Msekwa alisema ujio wa Rais John Magufuli umeleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi juu ya taswira ya chama hicho.

“Nafarijika kwamba uongozi mpya wa Rais anayetokana na CCM, Dk John Magufuli umeleta matumaini hayo mapya miongoni mwa wananchi walio wengi,” alisema.

Alieleza kuwa CCM kupitia viongozi wake, haina budi kuonyesha kwamba inaweza kuleta mabadiliko yenye tija na yenye kuleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi walio wengi.

Alisema ukongwe wa chama hicho kwa maana ya kuwa kimekuwapo na kimekuwa madarakani mfululizo tangu nchi ilipopata uhuru wake mwaka 1961, una faida na hasara zake.

“Faida ni kwamba kwa sababu ya uzoefu wake huo wa miaka mingi, kina (CCM) fursa kubwa ya kuendesha shughuli zake vizuri na kuendelea kupata ushindi katika chaguzi zijazo,”alisema.

Alibainisha pia kuwa kitendo cha CCM kuwapo madarakani muda mrefu kinaweza kusababisha hatari inayotokana na hulka ya binadamu.

Alifafanua kuwa wakati mwingine watu wanaweza kutaka mabadiliko tu ya uongozi wa nchi hata kama chama kilichopo madarakani kinafanya vizuri kiasi gani.

“Hatari iliyopo ni watu wanaweza kuchoka tu kuendelea kuwa chini ya uongozi wa chama kilekile na hatari hiyo inakuwa kubwa zaidi pale matendo ya viongozi wake yatakapokuwa mabaya kiasi cha kuwaudhi watu,”alisema.

Msekwa alisema katika kipindi hicho cha uhai wa CCM, maadili ya viongozi yameporomoka kwa kiwango kikubwa.

Alitaja sababu za kuporomoka kwa maadili kuwa ni pamoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini na ushindani mkali wa kuwania kushika dola uliojikita katika mfumo huo.

Alisema hali hiyo pia inatokana na hatua ya kusitishwa kwa mafunzo ya viongozi, makada na watendaji wa chama hicho yaliyokuwa yakitolewa kwenye vyuo mbalimbali.

“Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na kusitishwa kwa ruzuku iliyokuwa inatolewa na Serikali kwa chama kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo, katika vyuo vya chama vya Kivukoni na vyuo vyake sita vya kanda vilivyokuwa mikoa mbalimbali,” alisema.

Alisema kutokuwapo kwa msaada wa mafunzo ya maadili na uadilifu kwa viongozi, pia kulichangia kuporomosha maadili ndani ya chama.

“Hapo ilibidi kila kiongozi alazimike kutumia akili zake tu katika shughuli zake za uongozi. Kama wasemavyo Waswahili; akili ni nywele, kila mtu ana zake,” alisema.

Alieleza pia kuwa ushindani katika mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, umesababisha kukithiri rushwa katika uchaguzi.

Alisema hili hujitokeza wakati wa kura za maoni ndani ya CCM ambako baadhi ya makada wake wameanza tabia ya kuwashawishi wapigakura kwa rushwa ili wachaguliwe katika nafasi wanazozitafuta.

Alisema yapo mambo muhimu ya kuzingatia, wakati wa kutafakari chama hicho kilikotoka na kwamba katika kipindi chote hicho kimekuwa kikipata ushindi unaopanda na kushuka katika chaguzi zote zilizofanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.


Chanzo: Mwananchi
 
Wakati terehe 5 mwezi wa pili ni siku ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa Chama hicho, Pius Msekwa amechambua uwezo na udhaifu wake, akibainisha kuwa Chama hicho (CCM) KIMEPOTEZA SIFA YA ASILI YA KUWA CHAMA CHA WANYONGE.

Yaliyoathiri taswira ya Chama (CCM)
a. Migogoro baina ya viongozi, makundi yanayohasimiana.

b. Tuhuma za ufisadi kwamba CCM inakumbatia mafisadi

c. Wafanyabiashara kujipenyeza kwa kasi katika vikao vya Chama

d. Chama kupoteza sifa ya asili ya kuwajali WANYONGE.

chanzo: MWANANCHI
 

Attachments

  • IMG_20160204_071139.jpg
    IMG_20160204_071139.jpg
    341 KB · Views: 51
  • IMG_20160204_071030.jpg
    IMG_20160204_071030.jpg
    222.1 KB · Views: 54
Mzee msekwa namuheshimu sana huyu mzee

WAFANYABIASHARA KUJIPENYEZA KWA SPEED YA 4G KATIKA VIKAO VYA CHAMA
AHAAA connet dots.... ndo maana hata wakikwepa kodi tunawaomba walipe badala ya kuwashurutisha na kuwapeleka kwenye vyombo vya kutafsiriwa sheria km mahakama
CCM ni ile ile ooh ni ile ile
 
Wakati terehe 5 mwezi wa pili ni siku ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa Chama hicho, Pius Msekwa amechambua uwezo na udhaifu wake, akibainisha kuwa Chama hicho (CCM) KIMEPOTEZA SIFA YA ASILI YA KUWA CHAMA CHA WANYONGE.

Yaliyoathiri taswira ya Chama (CCM)
a. Migogoro baina ya viongozi, makundi yanayohasimiana.

b. Tuhuma za ufisadi kwamba CCM inakumbatia mafisadi

c. Wafanyabiashara kujipenyeza kwa kasi katika vikao vya Chama

d. Chama kupoteza sifa ya asili ya kuwajali WANYONGE.

chanzo: MWANANCHI
WATAMWAMBIA MZEE MSALITI NA ANAKARIBIA KUFA
 
Angetia neno kwenye haya yanayoendelea Zanzibar. Waishinikize chama Chao kitafute njia za kibusara zaidi kuliko kushinikiza uchaguzi. Vinginevyo kaongelea sifa za kawaida kabisa ambazo kila mtu anazijua kuhusu CCM.
 
Angetia neno kwenye haya yanayoendelea Zanzibar. Waishinikize chama Chao kitafute njia za kibusara zaidi kuliko kushinikiza uchaguzi. Vinginevyo kaongelea sifa za kawaida kabisa ambazo kila mtu anazijua kuhusu CCM.
kuhusu hali ya zenj wanagwaya kulisemea ila ikipatikana suluhu utaona watakapo jitokeza na kulitolea ufafanuzi sio kwa wanasiasa wakongwe pekee yao ni mpaka kwa wasomi na viongozi wa dini.
 
Mzee msekwa kaisha yupo kama kubenea tu mda wote kuwanza shanga na kuhangaika na mambo yasiyo ya msingi.
hahahahahaaa..kiukweli mzee kasema ukweli kama wanaccm wenyewe ndio nyie mzee ana haki ya kusema ukweli. ccm kimekuwa chama na pango la wanafiki na wazadiki.
 
Ameyasema hayo kwenye kitabu chake cha kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwa ccm. Amesema ccm imepoteza asili yake ya kutetea wanyonge

Chanzo: Magazeti ya leo

Waliosambaratisha azimio la Arusha ambalo ndilo lilikuwa msingi mkuu wa kutetea wanyonge na yeye Msekwa alikuwemo .Baada ya kusambaratisha akawa kwenye bodi ya kampuni ya kibepari ya vodacom kama mkurugenzi AKAINGIA KWA SPIDI YA 4G kwenye kampuni hiyo ya kibepari .Hawa wazee sio siri ndio wauaji wakubwa wa CCM Ile iliyokuwa ya wanyonge.

Azimio LA zanzibar MSEKWA alikuwemo na alihusika na liliua hasa asili ya CCM kuwa ya wanyonge.Hicho kitabu kaandika wengine kasahau kujiweka na yeye kama mhusika
 
Mzee msekwa namuheshimu sana huyu mzee

WAFANYABIASHARA KUJIPENYEZA KWA SPEED YA 4G KATIKA VIKAO VYA CHAMA
AHAAA connet dots.... ndo maana hata wakikwepa kodi tunawaomba walipe badala ya kuwashurutisha na kuwapeleka kwenye vyombo vya kutafsiriwa sheria km mahakama
CCM ni ile ile ooh ni ile ile
Oooh ni ile ile!
Viongozi ni wale wale!
ooh ni wale wale!
 
Kingine alichosahau si tu wafanyabiashara kujipenyeza kwenye vikao vya CCM kuliharibu chama lakini pia viongozi waliokuwa wa juu kama yeye kujipenyeza kwenye vikao vya bodi vya wafanyabiashara kama Vodacom AMBAKO YEYE ALIKUWA board member.Kujipenyeza huko kwa viongozi wa juu kama yeye kuliwapa GO ahead WAFANYABIASHARA NAO KUJIPENYEZA VIKAO VYA CCM kwa sababu ya hiyo kukaibuka UNHOLY ALLIANCE kati ya viongozi wa juu wa CCM na Wafanyabiashara wakubwa kwa pamoja wakaitengeneza CCM isiyojali wanyonge.

Msekwa kachangia hiyo hali
 
Tumeuziwa mbuzi kwenye gunia

Hata malaika Mbinguni WANAJUA kuwa ccm haina na haijawahi kuwa na nia ya kumkomboa mtanzania
We mwenyewe fikiria jitu fisadi linapewa uenyekiti wa bunge

lile fisadi lingine la CHADEMA lililohukumiwa na bunge kuwa fisadi la kutupwa CHADEMA mkalipa ugombea Uraisi unalisemeaje?
 
Back
Top Bottom