Msekwa amshukia Kingunge

Msekwa amshukia Kingunge

Nafikiri na wewe ukumsoma vizuri na kumsikiliza vyema. Kama unayo video rejea tena alivyosema. Kawasemea wote. Kamati ya maadili kupeleka majina matano haikuwa sahihi haina madaraka hayo. Alisema wote 38 walipaswa kufikishwa kwenye kamati kuu n kuojiwa (tena akasema maswali sinzaidi ya matatu). Najua na yeye anajua hawakutaka jina la lowassa lifike hata Kamati Kuu maana hawakuwa na uhakika kama litaweza kukatwa huko! Lakini kama ni kusemea alisemea wote siyo Lowassa pekee.


"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.

Hiyo hapo nimequote gazeti la Mwananchi....
 
kingunge yuko sahihi kwa hoja za kuikosoa ccm. tatizo tayari na yeye ana mgombea wake...
 
kumbe ni gazeti la Uhuru = CCM...

Hv mnalisomaga haya magazeti ya Nape...urojo mtupu...pumba bin ujinga
UHURU NI daily Order.
Kutokusoma ni makosa
IMEZUILIWA

Usha wahi kusikia hiyo mahali popote, au nyie ni wa udaku tu.
 
Wote wanaoitwa wazee ndani ya CCM ni janga kwa Taifa letu hakuna mwenye busara wala msekwa,wala kingunge,mkapa na wengine wote hamna kitu ni ujinga mtupu,wanaojiita wazee wa CCM si wakweli hata tone wamejaa uzandiki ,unafiki,na upuuzi wa kila aina kwa hata mambo yakienda hovyo husema yako vzr.Ukweli tuuseme bila kupepesa macho.
 
Kama kweli mzee Kingunge anatetea kuvunjwa kwa taratibu kwanini anakaa upande wa LOWASA tu....ina maana hizo taratibu zimevunjwa kwa kukatwa Lowasa tu....
Je kama taratibu zingevunjwa kwa kumpitisha Lowasa angesema maneno hayo.....??
Nina hakika kama lowasa angepita kwa taratibu hizo hizo mbovu wala asingelalamika na nisingemshangaa akimshutumu kada ambaye angelalamikia taratibu hizo hizo mbovu....
 
"Ukiona mtu anabadilika ujue amenunuliwa....."
Mtaturu Katibu CCM Mwanza.

Kama kweli mzee Kingunge anatetea kuvunjwa kwa taratibu kwanini anakaa upande wa LOWASA tu....ina maana hizo taratibu zimevunjwa kwa kukatwa Lowasa tu....
Je kama taratibu zingevunjwa kwa kumpitisha Lowasa angesema maneno hayo.....??
Nina hakika kama lowasa angepita kwa taratibu hizo hizo mbovu wala asingelalamika na nisingemshangaa akimshutumu kada ambaye angelalamikia taratibu hizo hizo mbovu....
 
msekwa mkewe jk alimpa ulaji katika jengo la ccm, mpaka sasa anakula kiulaini mama abdala. kama ulimuona kwenye mkutano mkuu msekwa alikuwa anamtetemekea jk. kingunge bahati mbaya huyu mzee huwa aogopi mtu kama wanafiki akina msekwa...nakumbuka hata huko nyuma alikemea baada ya kuona nyumba nzima ya kikwete ni wajumbe wa mkutano mkuu na akasema...CHAMA KIMEGEUKA MALI YA FAMILIA

Kwa hiyo kama Kingunge hazijui hizo kanuni kwa vile ni mpya jee na Nchimbi, Kimbisa na Sofia Simba nao hawazijui wakati ni wajumbe was KK?
Msekwa anyamaze tuu kwa vile CCM wameumbuka kupitia Kingunge
 
Kingunge si mjumbe wa kamati kuu wala halmashauri kuu hivyo yote aliyoyasema ni ya kuhadithiwa maana yeye hakuwemo kwenye vikao. Inawrzekana kweli alinunuliwa maana twaambiwa 1995 yeye ndiye alieongoza mashambulizi kwa Lowassa sasa amekuwaje mzuri sasa?
 
Ukisoma umetulia kauli ya Msekwa ni ya kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Kingunge kasema kanuni na taratibu zilizopo ambazo hazijahuishwa, mbona Msekwa hakusema zilibadilishwa lini?

Unataka kusema hata hao akina Nchimbi na wenzake ambao ni wajumbe wa kamati Kuu hawakufahamu hizo Kanuni zilizobadilishwa? Na hao akina Mtaturui wanaisdhi katika maisha ya zamani ambayo kilichosemwa adharani na mwenyekiti hapaswi kupingwa.

Ingawa mimi ni mmoja wa wale waliokuwa wanapinga kuteuliwa Lowassa lakini kwa maoni yangu huyu Mzee amejirejeshea heshima kwa jamii kwa kusimamia uvunjifu wa taratibu na kanuni.

Unamdaganya Kingunge azidi kuharibikiwa? MWACHE APOTEE UTEUZI ULISHAFANYIKA NA MAGUFULI NDIYE RAIS HAKUNA NAMNA WAPIGWE TU.
 
attachment.php



  • Asema hajui kanuni, amepitwa na wakati
  • Mtaturu(katibu CCM Mwanza): heshima ya Kingunge imeshuka

Makamu Mwenyekiti Mstaafu CCM Pius Msekwa amesema tuhuma zinazotolewa na mwanasia mkongwe nchini , Kingunge Ngombale Mwiru dhidi ya vikao vya juu vya chama hazina ukweli wowote.

Msekwa alisema, tatizo linalomkumba Mzee Kinunge ni kuganda kwenye utartibu uliokuwa ukitumika wakati yeye alipokuwa Mjumbe wa Kamati Kuu miaka mingi iliyopita

Aliongeza kuwa Mzee Kingunge hana habari na kanuni zinazotumiaka sasa na hajataka uzifaamu.

Katika hatua nyingine. Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza. Miraji Mtaturu, amesema Mzee Kingunge amejipotezea heshima aliyojijengea kwa miaka mingi kutokana na kauli zake.

"Nashangazwa na kauli iliyotolewa na Mzee Kingunge akiwatuhumu (wazee) kuendesha vikao vya mchakato wa kumpata mgombea urais kwa mizengwe na ajenda ya siri"

"Ukiona mtu anabadilika ujue amenunuliwa...!

Chanzo:
Gazeti la Uhuru😛 1, pg4

MY TAKE
Kingunge anatikisa mzinga wa nyuki!
(mods thanks for the clarity)

tuondolee habari za gazeti LA kufungia mandazi na bangi
 
Hakuna asiye jua babu ni fisadi...na anamtetea fisadi mwenzake..full stop...kinachomchanganya ni ahadi alizopewa na hela alizokula
 
Mchakato wa mgombea urais umehamia kwa wazee wa chama, wacha wagombane kwani ugomvi wa pazi furaha ya kunguru.
 
Huyo Msekwa ndo anajishushia heshima. Kingunge yupo sawa.
 
Kwa hiyo kama Kingunge hazijui hizo kanuni kwa vile ni mpya jee na Nchimbi, Kimbisa na Sofia Simba nao hawazijui wakati ni wajumbe was KK?
Msekwa anyamaze tuu kwa vile CCM wameumbuka kupitia Kingunge

Ukila vya watu na lengo halijafanikiwa ,hao wajumbe na babu Yao ni dhahiri waonyeshe hayo ,
Linashindikana vipi kutokuzujua hizo Kanuni si walikuwa na kampeni muda wote,
Ficha fedha ktk kitabu utakuta salama
 
Back
Top Bottom