MSD yaanza usambazaji wa vyandarua mkoani Kigoma

MSD yaanza usambazaji wa vyandarua mkoani Kigoma

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Baada ya kuanza zoezi la usambazaji wa vyandarua Mkoani Kigoma MSD leo imeendelea na usambazaji wa vyandarua hivyo huku leo hii ikikamilisha kusambaza kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma. Zoezi hilo linatarajia kuhamia Wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Hata hivyo, timu ya usambazaji imekutana na changamoto kadhaa ikiwemo Mto Lwiche ambao upo Manispaa ya Kigoma ujiji. Timu ya MSD imepaswa kutumia usafiri wa Boti na pikipiki kufikisha vyandarua takribani 500 kutoka mtaa wa Kanswa kwenda Ng’ambo Mtaa wa Mgumile.

Mwakilishi wa Menejimenti ya MSD (Mkurugenzi wa Ugavi – MSD) Bw. Victor Sungusia amezungumzia zoezi hilo baada kutembelea eneo hilo na kujionea changamoto za usafirishaji. Sungusia amesema Pamoja na changamoto hizi za miundombinu sisi MSD ndio jukumu letu kwani tutatumia aina yeyote ya usafiri kuhakikisha vyandaru hivyo vinawafikia wananchi kwenye maeneo yao ya ugawaji
1748506931960.png
1748506946502.png
 
Vimewekewa dawa ya kuua au kufukuza mbu?
utaratibu wa kugawa ukoje? Kwa kila mama mjamzito, au kwa kila mgonjwa wa malaria au kwa kila kaya moja neti moja?
 
Back
Top Bottom