Msanii Wema Sepetu arejea CCM, aitosa CHADEMA

Atawarudisha CCM kwa gharama yoyote ile ikiwemo kuwapa rushwa ya mamilioni au vyeo au kuwatishia kuwabambikia kesi nzito ili kuwatia hatiani na kuwaswekwa lupango.

Ni wazi kuwa watu wanarudi ccm sio kwa mapenzi ya moyo wao bali kutokana na vitisho vya jela au uharibifu wa mali zao. Sio wote wana mioyo migumu kama Mbowe ambaye unambomolea kitega uchumi, anaharibiwa shamba lake la kisasa huku watu wanapiga selfie ili wapandishwe vyeo na hujuma zingine lakini hababaiki.
Kwa hili huwezi kusifia ccm kuwa inavutia wananchi ili waiunge mkono bali ni uhalifu wa kisiasa na watu wanaenda huko kujiokoa na dhahma kwa maisha yao. Ni sawa na kumtaka mwanamke huku umeshika panga na akakubali kisha unajisifu unapendwa naye ndio maana kakupa ushirikiano wakati huo ni ubakaji.
CCM inambaka Wema kisiasa.
 
Asante sana malisa kwa kujitoa mhanga kumweleza mwenyekit wetu ukweli inauma sana watu waliopigania chama wanawekwa pemben then makap kutoka ccnjemu ndo tunayaona ya maana

Fly to kia baby
 
Bado Edo CDM haihitaji watu laini,Inawahitaji akina Lema,Msigwa,Heche,Suzana nk!Si sehemu ya kuuza sura wala kutafuta huruma!Amerudi kundini kuuza nyago akaungane na akina baba Tiffah!
 
Sumaye aliandaliwa kuwa mgeni rasmi ktk sherehe za kumpokea Wema ambapo yeye (wema) hata hivyo hakutokea!

Aibu sana hii.
 
Athari yake kubwa ni ipi chifu?
Inaonekana Chadema ni chama cha kukurupuka, viongozi hawajui kupima mambo kwa kuona mbele, kujua faida na hasara zake.

Chadema kimekua chama cha matukio badala ya ajenda, viongozi wake wanawaza kuuza gazeti tu.

Inabidi Chadema ya awali irudi, ile iliyoungwa mkono na wasomi wengi pamoja na raia wa kawaida tena kwa kujitolea.

Watanzania wengi tunapinga serikali ya Magufuli kwa ubabe wake, ila haimaanishi tunaunga mkono Chadema.....

Chadema ya sasa imepoteana haiamininiki wala haijielewi.....2020 baada ya upinzani kupoteza viti vingi vya ubunge ndio utaelewa ninachokiongea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom