Hatuwezi kuwa entertained na yasiyowezekana. Bongo movie wamezidi Utoto. Wananchi tunapiga kelele Polisi waache kubambikia watu kesi, lakini Bongo movie akiact kama Polisi anakwenda kumpekua mtuhumiwa wa madawa ya kulevya anamtoa nje mwenye nyumba halafu anapekua ndani akiwa Peke yake akikosa madawa anarudisha Taarifa nje Kwa bosi aliyemwacha na mtuhumiwa. Hata kama hatuwapendi Polisi lakini hawawezi kufanya ujinga huo. Lingine unakuta Bongo movie Askari mdogo labda Koplo anakwenda kumkamata RPC wake mla rushwa, hili jeshi gani Jamani au kuna mikoa RPC ni Konstebo? Ni vema waigizaji wakaigiza kitu sahihi ili kuifumdisha Jamii.Sio kila entertainment ni kufundisha, mengine ni entertainment for the sake of entertainment.
Shule ipi unayoimaanisha? Hii hii ya kumaliza form 6 na kwenda chuo kikuu? Kama ni hii, je kwa walimu wepi?Usanii bila shule ni ujinga mtupu.Joti ni std 7 yeye ni stearing,yeye ni Director yeye ni kila kitu unategemea final product gani !.
Nimeangalia clip yake ya maigizo inayoitwa(kazi na ngono)katika igizo hili limeanza vema lakini ktk kumaliza nadhani lina utata. Joti aliigiza kama binti mwenye elimu ya digrii anayetafuta kazi, lakini bosi akamtaka kimapenzi ili ampe kazi na aliposhindwa kugawa uroda bosi hakumpa kazi.
Joti akarudi nyumbani na kumsimulia mama yake na hatimaye yeye mama na mtoto wakaambatana kwenda ofisini. Na walipofika ofisini mama akamkamata roba bosi na kutoka naye nje halafu Joti akakalia kiti cha bosi ofisini na kuanza kutumia desk top kama mfanyakazi.
Sasa kwanini nasema amekosea, igizo lilipoanza lilikuwa linaashiria kufundisha kupinga unyanyasaji wa kingono toka kwa mabosi, rushwa ya mapenzi. Lakini limeisha kwa kuteka ofisi. Watalam mnisaidie hii ni sawa ktk kuwasilisha ujumbe?
😂😂😂😂😂Mkuu ulitaka afanyaje? Mbona wengine wanaimba rakatarakata reketerekete rukuturukutu na Bado wanalipa mkuu?
Kazi nafanya na huenda hadi nakuzidi wewe kipato.Wewe unayejuwa kuchambtwa kazi za sanaa tupe uchambuzi wako tujifunze.mleta mada una ubongo uliosinyaa sana.
Kwanza hujui kutafsiri kazi ya sanaa.
Pili nampongeza joti kwa kuleta conflict kwenye namna ya upokeaji ambapo ni kazi nzuri ya sanaa kumchanganya mpokeaji wa kazi ile.
Tatu heb fanya kazi mwenzako ashaingiza siku ww ndo kwanza unaleta malalamiko jf kwan hao youtube na media zinazoonyesha hawajachambua kwakajua kua inamafundisho au haina.
mkuu hapana,ila igizo lilivyoanza na lilivyoisha halijalenga ujumbe kusudiwa.Kwahiyo kilichokutisha hapo ni kipi?! Kwamba watu watateka ofisi wakiona hiyo video?!
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] siwezi kukupinga kwa mawazo yako[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kazi nafanya na huenda hadi nakuzidi wewe kipato.Wewe unayejuwa kuchambtwa kazi za sanaa tupe uchambuzi wako tujifunze.
Sio kila entertainment ni kufundisha, mengine ni entertainment for the sake of entertainment.