Msanii wa hip hop marufuku Srilanka

Msanii wa hip hop marufuku Srilanka

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Serikali ya Sri Lanka imempiga marufuku mwanamuziki wa kimataifa kutoka Marekani, Akon, kuingia nchini humo kufuatia maandamano yanayopinga kanda yake ya video inayoonekana kukejeli dini ya Budha.
Mwanamziki huyo mzaliwa wa Senegal alitarajiwa kuandaa tamasha lake kubwa mjini Colombo mwezi Aprili.

Video hio ya wimbo , Sexy Bitch, inaonyesha watu waliokusanyika karibu na bwawa la kuogelea kwa karamu maalum nyuma yake ikionekana sanamu ya Buddha .

Taarifa ya serikali ya Sri Lankan imesema kuchanganya sanamu hiyo ya Buddha pamoja na wanawake waliovalia mavazi yasio na sitara kumewasikitisha wafuasi wa Buddha kila mahali kwa hiyo maombi ya Akon ya kupewa visa hayatakubaliwa.

Zaiara yake ambayo ilitumainiwa ingewavutia mashabiki kutoka nchi nyingine za Asia imekwishazusha mgogoro mkali. Kundi la watawa wa kihafidhina limesema video za Akon hazifai kwa nchi yenye wafuasi wengi wa Budha kwa sababu inachochea hisia za ngono.

Mnamo siku ya Jumaatatu takriban watu 200 waliyashambulia kwa mawe na chupa makao ya kampuni moja iliyohusika na kuitangaza ziara ya Akon.

Akon amesema yeye ni mtu wa kidini ambaye kamwe hatathubutu kukashifu imani ya kidini ya mtu yeyote.
 
bora kidogo tusikie na ukali wa mabudha, bado wahindu manake kila siku ni ukristo na uislam tuu ndo nawasikia wakitaka kuonyesha machungu, afu wakimaliza hao tusikie na dini zetu za asili (kiafrica) zikicharuka kua wakuja (wazungu,waarabu na wahindi ) wametutawanya na kuvuruga dini zetu. mmmmh hapo patakua pazuri zaidi. ila najiuliza ikiwa wapo waafrica ambao tutakua tayari kwa hili........
 
Back
Top Bottom