2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,361
- 6,083
Historia ya kuunda Dola za kiislamu hazina mvuto, mfano Iran walifanikiwa kuunda lakini ni ya madhehebu ya washia, ambapo Kwa watu wa Suni wanawachukulia kama sio waislamu bali makafiri!
Saudis na nchi nyingine za ghuba ( Gulf Arab states ) zimejaribu kuishi kwa kufuata misingi ya kidini lakini kwa bahati mbaya bado zinaendeshwa kifalme, kitu ambacho hakipendezi kwa imani ya kiislamu, yenye kuamini kwamba Mungu anatakiwa amtawale binadamu. (Only God should rule over humankind).
Mfumo unaoundwa na Abu(Khalifa wa Dunia) hauna tofauti na mifumo iliyoundwa na Afghan Taliban au Ansar Dine, the North African jihadists wa Mali kuanzia 2012 . Ni wazi Udikteta unajionyesha kwenye nchi zenye kusimamia misingi ya kiislamu.ingawa nchi kama Syria na Talban(Afghanistan) ina unafuu kiasi kuliko tawala za kumwaga damu, kama ya Abu.
Abu si mtu wa kwanza kujiita Khalifa mpya tangu yule halisi na mwisho aliyemaliza mwaka 1924.Waislamu India na Africa wameshatangaza makhalifa wao katika vipindi tofauti kwa miaka 150 iliyopita ambapo wameishia kufeli kwa Aibu.
Miaka ya karibuni mataifa yalioibuka na kujiita ya kiislamu yamejikuta kwenye wakati mgumu na kuporomoka baada ya kutoa hifadhi kwa Magaidi, mwishowe mataifa yenye nguvu na uwezo kijeshi ya nchi za magharibi yamewazamisha na kuwafutilia mbali.
Hii ni changamoto ambayo Abu anahitaji kuiona uhalifa wake usitumbukie nyongo:
Abu na Saa Ya Rolex
Heshima mojawapi kwa mwanajihadi ni idealistic na kuonekana hayumbishwi na majaribu ya Dunia na anasa zake. Ikiwa watu wataanza kuhisi Abu ni mtu mpenda anasa na bling bling kwakuwa wanamwona anapiglia vitu vya gharama kubwa, kama kuvaa saa ya Rolex, ni wazi atakuwa na wakati mgumu aendako.
Kupiga marufuku miziki:
Waislamu wa Afghan na Malians wanapenda muziki kama sehemu ya utamaduni wao.Ikiwa Mziki utapigwa ban, kwasababu hauendani na Uislamu, basi ni wazi kuwa Ushawishi wa Abu utayumba. MfaNo, wanafuasi wake wamewatishia kifo kikundi cha wasanii wa muziki cha pop cha wa Kurdish.Mziki unajenga marafiki na kuhamasisha.
Kuadhibu wanawake kwa tuhuma za uvaaji usio na staha.
Waislamu wa Mali kaskazini walipochukua madaraka ilifikia wakati waliwakamata wanawake wengi na wasichana, na kuwaadhibu mbele ya wanaume. Meya waTimbuktu ( Halle Ousmane Cissé ) alilalamika kwa AnsarDine(kiongozi wa jihadists); mbona mnaibadilisha dini yetu kwenda kwenye dini nyingine, mnawatupia wake zetu na mabinti zetu kwenye nyumba na kisha mnawapiga mbele yetu? halafu mnataka tuwapende?. Wafuasi wa Abu wameanza kufanya hivyo tena.
Uharibifu wa vitu vya kihistoria.
Jihadisti wa Timbuktu waliharibu vitu vingi vya kihistoria wakisema haviendani na Uislamu na mafundisho ya Uislamu(Un-Islam). Wenyeji wakachukulia siriaz kuwa yale ni matusi ya mila na utamaduni wao.ikiwemo kuua sehemu za utalii za Timbuktu.Wataliban waliharibu masanamu ya budha (Bamiyan Buddhas) hii iliamsha hisia kali kwa jumuia ya kimataifa. Abu ameharibu tomb of Jonah(NAbii Yona aliyemezwa na Samaki) Ilifika wakati wanamji wa Mosul walizunguka maeneo na kuunda ring ilikuzuia yasiharibiwe. Hii ni ishara kuwa hawaridhiki na mambo yanavyokwenda.
Jeshi la Abu lenye mchanganyiko na wageni(foreigners) ni shidaa:
Wa-Syria na waIraqi wanaukubali utaifa wao kama vile wafanyavyo Waislamu.Sababu moja ya makabila yaIraqi kupambana na AlQaeda mwaka 2006, ni kwasababu wageni walionekana kuwafundisha wenyeji namna ya kuishi.(Anbar Awakening).
Japo Wamarekani waliwachukiwa sana lakini hawakusema wanataka kuoa wanawake wao ama kuleta itikadi zao za kidini kwa wenyeji.Hii ikawafanya makabila haya waone wamarekani sio waovu sana kwao kuliko Alqaeda, Mwishowe wenyeji wakaungana nao kuwapiga alqaeda.
Pia Timbuktu ilikuwa ngumu kuwaunganisha wasio waafrika na wasio waarabu waliokuwa sehemu yajeshi la Ansar Dine. Kuna madai pia kwa Abu matatizo yameanza kujitokeza kwa waSyria.
Ushirikiano na watu maarufu(Local Elites):
Sababu mojawapo ya waIraqi kuwageuka Alqaeda ni ushawishi wa watu maarufu katika makabila ambao waliwachoka alqaeda. Huwa ni kawaida ya waislamu wanapotawala eneo hawataki chalenji kwenye mamlaka yao. Hii tabia inaweza kupelekea Local elites kuanzisha ushawishi kwa jamii kwamba wananyonywa na wageni na wakaanza mapambano ya kujikomboa.
Mfano Afghanistan kabila la wa-Pashtun kiongozi wao mmoja aliwageuka alqaeda na kuungana na wamarekani.Hali inajonyesha kwa mashekh kaskazini mwa Iraqi wameshaanza kuchoka kushirikiana na Abu dhidi ya serikali wanayoichukia ya Baghdad.
Kupiga marufuku Starehe:
Watalibani walipiga marufuku utamaduni wa afghanistan wa kurusha tiara(kite flying),Wairan walizuia Tv na satellite antenas, na Abu inasemwa amepanga kupiga ban uvutaji wa Sigara.
Kueneza ubaguzi miongoni mwa waislamu:
Wapiganaji wa kiislamu wa Libya walipoteza mashiko kwa kulipua Kaburi la watakatifu Sufi wakiwalaumu kuwa waislamu wa Uongo( Salafists as examples of "false Islam). Ajabu ni kwamba waislamu wa Libya wanajisikia kama wako nyumbani na hao wasufi kuliko sere na Salafism ambapo waislamu wapiganaji walionekana wakijaribu kuung'oa. Walibya walipiga kura kuwaondoa hawa waislamu wapiganaji popote walipopata chansi. Na sasa Abu baadhi ya Alqaeda wanasapotiana na washiite dhidi ya Abu.
Ni wazi kwamba marehemu Ayman al-Zawahiri, na msaidizi wake Osama bin Laden's watakuwa wanalaani utawala wa Abu, pia wazi jihadi movement itaishia kizani kwa aibu .
Abu Kujiita khalifa(Caliph)
Kuna migawanyiko mingi kwenye namna ya kuwaunganisha waislamu wa Sunni.NA ni wazi kuwa kila msunni angetamani kuona cheo cha ukhalifa kinarudishwa. Hata wale waliozama kidini (Zealots) watakuwa na mawazo tofauti namna cheo hicho kirudishe.Kitendo cha Abu kujitangaza yeye ni khalifa ni wazi kuwa kinaamsha Hasira kwa watu ambao pengine wangeweza kuwa upande wa Abu.
Waislamu ulimwenguni kote wangependa wawe na utawala wa kiislamu. Wengi wanapenda idea ya sharia na taratibu, haki na kusimamia sharia zinazokwenda kinyume na rushwa(Corruption) na viongozi wakatili ambao wengi wao wanaongoza hizi nchi zinazojiita za kiislamu lakini ni za kifalme.
Lakini hata wale wenye lengo la kutimiza ndoto hii wamekuwa wakitanguliza ubabe, kulazimisha na ukatili ili kufikia lengo.Matokeo yake inapelekea machafuko na mivurugano katika mkakati mzima.
Kwa Abu kujiita khalifa ni wazi kwamba anataka kuaminisha kwamba anaweza kuwaunganisha watu na Dunia ya waislamu na kuzuia upinzani utakaojitokeza kwake.
Taswira tofauti na matarajio ya Abu kwani unyanyasaji wake wa jamii ndogo ya wakristo wa monsul haijamsaidia kufikia ilo lengo duniani.
Gepu ni pana sana kati ya kinachohitajika(Ideal) katika Uislamu na kile kinachoenda kumalizikia kwenye eneo ISIS . Ipo Haja ya Abu kusikiliza ushauri kutoka kwa watu anaotaka kuwatawala, asikilize kile wanachosema,ni wazi anaweza kushangazwa na kile watakachosema.
Source:foreignpolicy