Tetesi: Msanii Rashid Abdallah Makwiro 'Chid Benz' ajiunga katika lebo ya WCB

lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
992
904
Msanii maarufu wa miondoko ya kufoka/kurapu Rashid Abdallah Makwiro al maarufu kama CHID BENZ amejiunga rasmi katika lebo ya Wasafi Classic Baby WCB mchana Iliyo chini ya mwanamuziki machachari kabisa Diamond platnumz.

Taarifa hizi zimepatikana kupitia mtu wa karibu sana wa Babu Tale. Na pia kituo cha kuaminika cha redio yaani CloudsFM kimetaarifu mchana huu.
 
Naona taratibu dogo Mondi ana transion kutoka kwenye u entertainer na kuelekea kwenye u music mogul.

Kwa kweli juhudi za huyo dogo nazipenda maana kaweza kujikwamua kutoka kwenye hali duni sana ya kimaisha hadi kufika hapo alipo.

#Positivity#
 
WCB isije kuwa kama kokoro, linakusanya kila kitu, Kenge, Kaa, Samaki na kila kiumbe cha majini.

Katika kutaka kujitanua na kubeba wasanii wengi wanatakiwa kuchuja. siyo kila aina ya Msanii ni wakusajiliwa na Label hiyo. Nadhani mpaka kufikia hapa wameshajipapambanua ni lebal ya namna gani na wasanii wa aina gani.

Waangalie, kunawasanii wanaweza kuiangusha lebo yao kwa namna moja ama nyingine.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom