Msanii Pharell: Ni marufuku kwa Rais Trump kutumia wimbo wangu kwenye siasa, ukiendelea nitakuburuza mahakamani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
pharrell-williams.jpg


Mwanamuziki na Muandaaji wa muziki nchini Marekani, Pharrell Williams amemlima barua Rais wa Taifa hilo, Donald Trump inayomtaka asitumie tena wimbo wake wa ‘HAPPY’ kwenye shughuli zake za kisiasa.

Pharrell amechukua maamuzi hayo, baada ya Rais Trump kuutumia wimbo huo Wikiendi iliyopita katika Mkutano wake wa Kisiasa mjini Pittsburgh katika eneo ambalo masaa machache yaliyopita kabla ya mkutano huo, kulitokea mauaji ya watu 11 katika Sinagogi la Wayahudi.

Siku hiyo hiyo ndani ya eneo moja, watu 11 wameuawa halafu masaa machache unacheza wimbo wa Happy inaingia akilini? tena kwenye masuala ya kisiasa. Sisi kama wanasheria tumeafikiana na Mteja wetu kuwa Rais huyo asiutumie tena wimbo huo na akirudia kufanya hivyo tutampeleka mahakamani kwa makosa ya Copyrights na ‘trademark rights’,“ameeleza Mwanasheria wa Pharrell Williams aliyejitambulisha kwa jina la Howard King.

Mwanasheria huyo amedai kuwa kitendo cha Trump kucheza wimbo huo jukwaani, ni kitendo cha kichochezi na kina weza tafsiriwa vibaya kwa wananchi wa eneo la Pittsburgh huko Indiana.

Kwa muda mrefu Pharrell (45) amekuwa akikipigia upatu chama cha Democratic, ambacho ndio chama pinzani kikubwa nchini Marekani dhidi ya Chama tawala cha Republican cha Donald Trump.
 
Pharrel tangu enzi hizo mzee wahenga tupo nae,lakini he is still young till now,sisi wala vumbi pamoja na kutupita umri tumeshapauka tayari kama vile vipande vya mihogo mibichi aisee,pesa sabuni ya roho anyway,wenzetu demokrasia ipo juu sana kila mtu anaruhisiwa kutoa maoni,povu,wazo kuhisiana na jambo lolote lile kwa mamlaka yoyote au mtu yeyote yule ingekuuwa huku angeshatekwa na kupotezwa huyo bongo nyoso sana shit...
 
Hii nchi ina uhuru wa ajabu, wavuta bangi kina Snoop wanamtukana kila mara ila Rais hana habari nao, kweli US ni US
 
Back
Top Bottom