Msanii Ney wa Mitego kujenga kanisa

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
518
613
Msanii wa mziki wa kizazi kipya NAY WAMITEGO amesema kuwa yeye yuko mbiyoni na wazo la siku za usoni, kujenga kanisa nakulimiliki yeye mwenyewe .

Alipoulizwa sababu ya kujenga kanisa msanii huyo amejibu: kanisa ni biashara inayolipa kuliko biashara nyingine, kwa hivyo lengo lake kubwa ni kuongeza kipato.

======================================
Msanii wa muziki Nay wa Mitego amesema kuwa ana mpango wa kumiliki kanisa siku za usoni kwa kuwa anaamini kwa sasa dini ndiyo biashara inayolipa zaidi ndani ya nchi na Afrika kwa ujumla.

Kauli hii imetoka kinywani mwa Nay wakati akijibu maswali ya mashabiki kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, baada ya kuchana mistari kadhaa iliyomo ndani ya ngoma yake mpya aliyoiachia leo mistari inayosema

Amesema kuwa kuwa yeye anatarajia kuwa mmiliki wa kanisa la imani anayoiamini yeye menyewe na kuongeza kuwa hiyo ni biashara inayolipa zaidi kwa sasa.

"Broo wewe kama una kiwanja chako jenga kanisa ni biashara inayolipa sana. Mimi natarajia siku za karibuni nitakuwa mmiliki wa kanisa kwa dini ninayoiamini mimi. Sitakuwa mchungaji lakini nitakuwa mmiliki wa kanisa" Nay aliwaeleza watazamaji wa KIKAANGONI.

Nay 'The true boy' ameongeza kwamba katika orodha ya matajiri kwa sasa barani Afrika ni viongozi na wamiliki wa makanisa.

Chanzo: EATV
64a1f697283f622df2531c522fb8844b.jpg
ffc0931d0bce3b1028ce175e44552e17.jpg
4d7740d2ca3f0365436379b2043ce6fa.jpg
 
Isije kuwa kuna single ikimbioni kutoka.....maana kama unajenga kanisa kama biashara sasa ikitokea waumini wako vipato vyao ni kidogo utaweka na kianzio cha kutoa sadaka n.k
 
Kuna Siku hyo ney alihojiwa na redio moja anasema hamini kwenye mambo ya dini wala kanisa

Ova
 
Hebu fikiria Mhubiri anakuwa Nay pale mbele
Waimbaji ni Vanessa, Dayna, ruby na jux
Wanakusanyaji wa sadaki ni weusi
Mchungaji msaidizi ni diamond
Wapigaji wa vyombo barnaba, ben paul na belle 9
Kisha mzee wa kanisa ni Alikiba
Mzee wa kanisa msaidizi ni Ommy dimpoz
Wakaribishaji wa wageni ni wema, Nandy, wolper, Tunda, Hamisa
Kisha wanaopiga beat za nyimbo ni dj fetty, zero
Na mchovu ndio kiongozi wa ratiba ya kanisa

Wewe lazima kila jpili uhuzulie church tu
 
Mimi hapa mtaani, Kuna jamaa alikuwa dalali baada akaingia bongo movie huku akiendelea na udalali wake sasa miaka kama minne sijamsikia, sasa juzi ndio nambiwa ana kanisa kimanga na yy anakula vichwa na hali si mbaya anausafiri wa ukweli.
 
Isije kuwa kuna single ikimbioni kutoka.....maana kama unajenga kanisa kama biashara sasa ikitokea waumini wako vipato vyao ni kidogo utaweka na kianzio cha kutoa sadaka n.k
Katoa song mpya inaitwa MUDA WETU ndo anaitafutia promo
 
Hebu fikiria Mhubiri anakuwa Nay pale mbele
Waimbaji ni Vanessa, Dayna, ruby na jux
Wanakusanyaji wa sadaki ni weusi
Mchungaji msaidizi ni diamond
Wapigaji wa vyombo barnaba, ben paul na belle 9
Kisha mzee wa kanisa ni Alikiba
Mzee wa kanisa msaidizi ni Ommy dimpoz
Wakaribishaji wa wageni ni wema, Nandy, wolper, Tunda, Hamisa
Kisha wanaopiga beat za nyimbo ni dj fetty, zero
Na mchovu ndio kiongozi wa ratiba ya kanisa

Wewe lazima kila jpili uhuzulie church tu
hii comment ni nyoko
 
Mkuu wewe Anakuona
 
Siyo wazo baya kwan iman sahv imetoka makanisani kilichobaki ni biashara na mambo mengne mazto.

Big up ney(nyambara gwa bhandu)
 
Back
Top Bottom