Wakazi ahukumiwa kumlipa Baba Levo Tsh. Milioni 100 kwa kumchafua

Wakazi ahukumiwa kumlipa Baba Levo Tsh. Milioni 100 kwa kumchafua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyopo Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hukumu katika shauri la madai ya kashfa lililofunguliwa na msanii na Mbunge Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) dhidi ya Webiro Wasira maarufu kama Wakazi.

Katika hukumu iliyotolewa tarehe 13 Machi 2026, mahakama imebaini kuwa taarifa zilizosambazwa na Wakazi dhidi ya mlalamikaji zilikuwa za uongo na zenye kumdhalilisha, na zimeathiri sifa yake katika biashara pamoja na tasnia ya muziki ndani na nje ya Tanzania.

Mahakama imeamuru mshtakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya shilingi milioni 100 (Tsh 100,000,000) kutokana na madhara yaliyosababishwa na taarifa hizo za kashfa.

Aidha, mahakama imeagiza mambo yafuatayo:
  • Mshtakiwa aombe radhi hadharani kwa taarifa za uongo alizosambaza.
  • Aondoe na kukanusha taarifa hizo katika tovuti, mitandao ya kijamii, blogu, magazeti na hata kwenye chaneli za YouTube.
  • Amezuiwa kuendelea kusambaza taarifa zozote za kashfa dhidi ya mlalamikaji katika siku zijazo.
  • Kiasi hicho cha fedha kitalipwa pamoja na riba ya asilimia 7 kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu hadi kitakapolipwa kikamilifu.
  • Pia gharama za kesi zimelipwa na upande wa mshtakiwa.

1773390728521.png

1773390739610.png

1773390749026.png
 
Wakazi hana hela ,ni wale diaspora wanaishi nje bila ya mpangalio wa familia kama Roma..Maisha ya huko ni magumu so familia wanaacha mbali .

Mtu mzima amebaki kushangaa maghorofa ,haya sasa kayatimba...

Ramadhani Mubarak.!
 
Back
Top Bottom