GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Msanii maarufu wa bongo flava Joseph Haule aka Proffesor Jay, leo hii amejiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kukabidhiwa kadi yake ya uanachama mjini Dodoma.
View attachment 94612 View attachment 94613
Hilo haliwezi tokea na kama ikitokea yatakuwa makosa makubwa mno, wasiwasi wangu ni kuona chama cha upinzani kikiwa na idadi kubwa ya wasomi wa level ya form ambao kiuhakika hawawezi kuiwakilisha vizuri nchi yetu hasa katika mambo ya msingi hasa kusaini mikataba mbalimbali otherwise watakuwa wapigadomo tu ila katika utendaji wataboronga.
Sasa Mkuu wa Kaya anavyopenda Bongo flava atasikiliza za akina nani? Na CDM now ni ya wasaniiii auuuuu
hapo prof jay anamwambia jk "aikemee serikali yake katika madudu inayoyafanya".
Lakini jk alidhani masihara, ikabidi jay ahamie kwa watu wanaotaka ukombozi wa kweli.
Cc: mohamedi mtoi, molemo, @crushwise, bujibuji, ben saanane, ndibalema
Bado Master J na Salama.Naona hamna aliyemkaribisha JF!
Jay, kama umeingia rasmi kwenye siasa za wazi na mapambano ya hoja pia tunakukaribisha JF.
Kuna wadau watakupika hapa, pia utaweza kuiona kwa upana siasa ya tz tokea kwenye jicho la mitandao ya kijamii.....
Msanii wa bongo fleva mwenye mvuto na kupendwa na watu wote ni Diamond, wengine hakuna kitu kwa sasa. Na yeye ndiye anaye ongoza kwa kipato ndani ya bongo fleva. Prof. Jay hakuna kitu tena, ni oil chafu hiyo mkuu
Kapima na kuona ni wapi panamfaa kuwepo,ni uamuzi wa makini na ni mfano bora kwa vijana wanamuziki ambao muda mwingi wamekuwa wakitumika kwenye majukwaa ya chama fulani bila kufanyiwa kile wasanii wanachokitaka,natumai kuwepo kwake CHADEMA atapambana vizuri kuhakikisha kazi za wasanii zinawasaidia na kuwaendeleza wasanii.
Karibu kamanda Joseph kwenye mapambano ya kuikomboa nchi yetu.
Mbona unaongea mengi aisee!!!Tatizo nini kijana mwenzetu??Prof J. ni legendary wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, historia inasema hivyo na itaendelea kuwa hivyo! Si busara hata kidogo kumlinganisha gwiji huyu na chipukizi wanaojitokeza sasa. Kazi za sanaa zina generations! Prof J na Sugu sio wa generation hii katika tasnia ya muziki wa Bongo Flavor
Huyu alikuwa ameisha jiishia zamani, hana tena Dili ndani ya muziki wa bongo fleva, alikuwa hana option zaidi ya hiyo , ili kujiliwaza kwani hata ndani ya medani ya muziki wa kizazi kipya hayumo tena , wakina Diamond wameisha mmaliza na kufanya jina lake lisahaulike. Kwa heri, kwa heri baba, kila wafu huzika wafu wenzao.
hii habari imenishtua sana ckuitegemea, nilitegemea j kujiunga na ccm jinc alivyokaribu na jk