Msanii jela miaka 10 kwa kumiliki fisi

Huyo fisi hafiki hata Bilioni, kafungwa miaka 10
Wale waliopoteza 11bil miaka 2

Imepunguzwa kaka.Mahakama ilisikiliza rufaa ya waliotusababishia hasara ya billion 11 yaani shilingi milioni elfu kumi na moja na kupunguza adhabu yao kutoka miaka mitatu mpaka mwaka mmoja.Na kuna uwezekano wakapata msamaha.
 
Huyu lazima alionyesha ushabiki kwa ukawa. Amekuwa na hao fisi muda mrefu tuu, amekuwa akitumiwa katia sherehe na shughuli nyingi za serikali na hajawahi shauriwa kuhusu hao fisi.
 
Ni vipi hakimu ameshindwa kutumia adhabu ya chini (sheria inawapa uwezo mahakimu kutoa adhabu ya chini) ukizingatia huyo msanii amekiri kosa, alikuwa anatumia fisi kwenye public na pia ni asili ya tamaduni za hapo
 
Ukigonga fisi mikumi nadhani ni chini ya us dola 150 au gharama ya kugonga na kukutwa inatofautiana..ubinadam hapo haupo uwezi mfunga binadamu miaka 10 kwa kukutwa na fisi walio hai..wanyama wetu wapo kila pembe ya dunia hakuna aliekamatwa wala kufungwa.
 
Hivi vitu ndio vinatia hasira wananchi... Haki ya nani ngoja october, 25 ifike. There is no rationality kabisa
 
Yaani faini 4800000 tsh halafu ukikosa miaka 10, ndo maana wenye pesa wanaweza teka wanyama wakauza wanapotaka halafu unalipa 4800000, Hivi sheria za namna hii zilitungwa na nyerere kweli!
 
Duuu tshs .4840,000/ten yrs more than 11bilion hasara 2yrs gerezani hivi hawa mahakimu ni kitu gani wanazingatia kumuhukumu mt anaeitia hasara serikali

Kama inakubidi utoe hukumu namna hiyo, namshukuru mungu sikuwa mwanasheria
 
Ccm out,baada ya huyu jamaa kusaidiwa vifaa vya kuwalinda na kuwatunza hawa fisi basi yeye anafungwa khaaa
 
Niuonevu huo kwanza mtanzania na hajawauza nje hao fisi wanaachwa wanaosafilisha twiga wetu nje hao waarabu na wachina wanao safirisha meno yetu ya tembo unamkamata na kumuhukumu msanii ambaye hana lolote lile badala ya kumuelimisha unamfunga huku familia yake ikitaabika mm amakweli hiyo ndiyo serikali ya magamba chini ya jemedari kinana.

Huu nimuonevu kupita maelezo. Kuacha siasa pembeni hii wahusika ni hao waliomuhukumu.Jamani kuna mambo yakitamaduni na yaliacha kuwa ya kitamaduni. Serekali imecxhukua hatua gani kujulisha wananchi kuwa hilo ni kosa? Kama alivyosema mwenyewe alikuwa anawatumia kuwaburi=udisha watu. asa hapa watu wa haki za binadamu ndio walitakiwa kijutokeza laikini wako mbele kutetea mafisadi kuchukua nchi kwa maslahi yao! Wazalendo wanatutoka Sijui Tanzania miaka kumi ijayo itakuwaje?!?!?!
 
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi, wewe mwenyee , ndugu, marafiki au wafanyaazi wenzko watasoma hapa!!!! Moyoni mwako ( acha shera maana uatasea ooh muata sheri) unaamini umetenda haki. Na CCM haya mambo dio yanayojnga chuki kwa wananchi!
 
Maskini pamoja na mafisiemu kumtumia kwenye mikutano yao wameshindwa kumsaidia kulipa hiyo faini.
 
Niuonevu huo kwanza mtanzania na hajawauza nje hao fisi wanaachwa wanaosafilisha twiga wetu nje hao waarabu na wachina wanao safirisha meno yetu ya tembo unamkamata na kumuhukumu msanii ambaye hana lolote lile badala ya kumuelimisha unamfunga huku familia yake ikitaabika mm amakweli hiyo ndiyo serikali ya magamba chini ya jemedari kinana.

This is not acceptable! Huyu hakimu aliyemuhukum hii dhambi itamuhukumu!!!!! o innocent local dancer unaenda kumfunga tena miaka kumi for his his ignorance?!?!? Na amesama mwenyewe kuburudisha watuna kujiongezea kipato. Mbona kuna ngoma wahindi huwa wanakuja na tembo (nakuelewa waliomba kibali) lakini umeshindwa kumuelemisha huyu baba wa watukuwa inabidi aidha awarudishe fisi hao au akaombe kibali? Kweli unakuwa naujasiri wa kutamka miaka kumi jela kweli?Hivi mnawataka nini watu hali ya chinihasa??? Elimu hakupata na si kuwa hakuwa na uwezo wa darasani ni fursa tu alikosa. Fursaza kazi kama yako hawapatiwi??? Rais atakayekuja aanze kushughulika na huyumama !!! Utakuta hapohapo kesi za ajabu watu wanaachiwa hapana. Let us join andfight for this innocent man on behalf of his family including: his wife,children and his extended family!

 
mkuu mie naunga mkono hoja, tutafute wakili wa kumtetea ili aweze kukata rufaa huku tukichanga pesa ya kumlipia faini yake, pia tumkatie vibali vya kufanya maonyesho ya fisi, watu wengi wanaamini matumizi ya fisi ni kwa ajiri ya ushirikina kumbe hakuna cha ushirikina ni sanaa tu.

Itasaidia pia kuondokana na imani potofu za uchawi na itasaidia kuokoa maisha ya wazee na albino wanaouliwa kwa imani za kichawi.
Naunga Hoja tuungane tupambane na uonevu kwa vitendo. Naomba organizers wa kukusanya michango waanzishe thread mpyamahsusikwa ajili hiyo kwani ikiunganisha humu tunaweza kuimiss. Uonevu huu haukubaliki!
 
ma.sisiemu.sio watu... huyu hakimu.ni mwehuuuuuu...

chenge anagonga na kuua watu mnamuacha..

huyu maskini traditional dancer mnamhukumu.... nyinyi ipo siku yenu
 
Vipi wale wanaoletwa kwenye show za akina Kinana na Chama chake wanakibali?.

Miaka Kumi kwa kosa kama hilo kweli Sheria iko kwa ajili ya wanyonge!Fisi wa 4.8milioni mtu ankwenda jela Miaka Kumi wakati fisi hao walikuwa wanatumika kujipatia mlo wa siku.

Kuna uwezekano hapo fitina ndiyo imesababisha hayo.
 
Naunga Hoja tuungane tupambane na uonevu kwa vitendo. Naomba organizers wa kukusanya michango waanzishe thread mpyamahsusikwa ajili hiyo kwani ikiunganisha humu tunaweza kuimiss. Uonevu huu haukubaliki!

Mkuu nami naunga mkono hoja ya mchango siasa zikae pembeni hapa..
 
Back
Top Bottom