Msanii jela miaka 10 kwa kumiliki fisi

Msanii jela miaka 10 kwa kumiliki fisi

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,795
Reaction score
5,255

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, imemhukumu msanii wa ngoma za asili, Mng'ahwa Kazanza (42), kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kumiliki fisi wawili na kuwatumia kwenye sanaa zake bila kibali.

Awali akisomewa mashtaka katika mahakama hiyo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo Septemba 28, mwaka huu, kwenye Kijiji cha Sisu wilayani Misungwi, majira ya saa 7:30 mchana, Mng'ahwa Kazanza (42) alikamatwa akiwa na fisi wawili wenye thamani ya Sh milioni 4.8.

Mara baada ya kusomewa mashtaka, msanii huyo alikiri kosa hilo na kudai alikuwa akiwatumia fisi hao katika sanaa zake bila kutambua kama ni kosa kuburudisha mashabiki wake kwa lengo la kuongeza kipato.

Kutokana na kukiri huko, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi, ilimtia hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali kinyume cha sheria Na. 5 ya mwaka 2009 na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa faini ya Sh 4,840,000 ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaomiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Msanii huyo alishindwa kulipa faini hiyo na hivyo kwenda jela kutumikia adhabu hiyo ya miaka 10.

Chanzo: Mtanzania
 
Jamani si angechangiwa hizo 4m/=+ ili azidi kusaidia familia yake kuliko hiyo miaka yote
 
Mramba na Yona wamehukumiwa mwaka mmoja kwa kufanya ubadhirifu wa mabillioni ya fedha

Unaona eh waje wakae hata wapitie uwiano wa adhabu hapo , bilioni 11 miaka miaka miwili ya kigereza, milioni 4 miaka 10
 
Mramba na Yona wamehukumiwa mwaka mmoja kwa kufanya ubadhirifu wa mabillioni ya fedha

Niuonevu huo kwanza mtanzania na hajawauza nje hao fisi wanaachwa wanaosafilisha twiga wetu nje hao waarabu na wachina wanao safirisha meno yetu ya tembo unamkamata na kumuhukumu msanii ambaye hana lolote lile badala ya kumuelimisha unamfunga huku familia yake ikitaabika mm amakweli hiyo ndiyo serikali ya magamba chini ya jemedari kinana.
 
haki iko wap kama tembo wanauawa kila siku meno yanaenda ughaibuni,twiga wanapanda ndege watuhumiwa wanaangaliwa .uyu ku2mia fisi akiwa hai hata elimu hana hajui kama kosa uku tatitz likiwa ni kujikwamua kutokana na umasikin ulosababishwa na ccm unamhukumu miaka yot hiyo.mungu huwa analipa hapa hapa duniani.
 
Wanyama pori kama simba chui nyati pundamilia, huwezi kuwafuga na kutembea nao kama mbwa.

Fisi wapo aina mbili, wapo ''mlulu'' hawa ni fisi pori na hawafugwi na ndio wanaokaa serengeti.

Huyu ni fisi wa kufuga kama mbwa ngombe paka, anaitwa ''nhawa'' huyu anaishi majumbani na anafugwa na kama uzito wako ndogo unaweza mdandia akakubeba kama punda au ngamia, hivyo huyo fisi sio nyara ya serikali haishi porini kama twiga au simba.

Wapo pia pakashume ambao hawafugwi na wanaishi porini na wapo ''nyau'' hufungwa na kuishi na binadamu.

Wapo ''mbwa mwitu'' hawa hawafugwi lakini tunao mbwa wa kawaida tunaofuga basi kama ni hivyo watu wanaomiliki paka na mbwa wakamatwe.
 
mkuu kwa hiyo hawa fisi wa aina hii ndo hawa wanaotumiwa na wachawi na kufugwa majumbani?
 
CCM wameshindwa kumsaidia msanii wao hadi anafungwa?
ImageUploadedByJamiiForums1443859001.786798.jpg
 
Wanaobeba wanyama hai mchana kweupe na wanaowapukutisha tembo wetu sidhani kama hawajulikani, lakini wanaishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom