Msanii Hussein Machozi anayeishi Italia adai watu weusi wakiugua corona hawatibiwi

Isije ikawa sababu ni weusi wageni wasio na bima..., hence ubaguzi ni kipato na sio rangi (ambao hata huku upo)
 
Norway ni nchi inayoifadhili ama kutoa msaada mkubwa Tanzania kuliko Taifa lote Duniani wangekuwa wabaguzi kiasi hiko hiyo misaada wanatoa yanini?

Tatizo lenu watu mnaoishi Africa mmekuwa na tabia za kiarabu mkienda ulaya au America au taifa lolote lenye freedoms hadi zimepitiliza mnafanya invasions na hamuwi assimilative hicho wazungu hawakipendi wanaogopa sana maana wanajua ancient wao walifanya nini
Na wale wachezaji weusi wanaozomewaga na kutupiwa ndizi uwanjani ni ivansions gani wanayofanya mpaka kutendewa vile? Na katika hilo la misaada, hakuna msaada wa bure anaotoa mzungu kwa africa bila kuwa na faida kwake! Acha kujifanya mtetezi wa waitaliano, wale kavu tu! Acha wafe
 
Dah!.. yaani sisi tunaomba huu ugonjwa upotee ili maisha yarudi halafu wewe unaomba uendelee kuua binadamu wenzako?

Unafikiri huu ugonjwa ukihamia Marekani na Israel wewe utabaki salama?
umeshawahi kusikia kuhusu ebola?

waafrika walikufa kama mchwa hapo kongo na afrika magharibi

huu ugonjwa uliundwa kwenye maabara za US, nini lilikua lengo lao?

vipi kuhusu ukimwi ambao unamaliza maelfu ya waafrika?

NB: KUNA WAKATI HURUMA INAKUJA ILA NIKIWAZA NJE YA BOX NAONA HATA HUU WAMETENGENEZA WENYEWE, THEN UMEWAGEUKA, SASA WAO HAWAKUUMBWA NA MSHIPA WA HURUMA HADI MAJARIBIO YA EBOLA WAJE KUFANYIA KONGO?
 
Mkuu,huyo Hussein Machozi anaingia kwenye kundi la vijana wale ambao wakitoka nje ya nchi na akakosa kitu kidogo anakumbuka Tanzania na haishi kulalamika kila muda.

Kazoea angekuwa huku mara aonane na Mwajuma, Jioni akale chips zege na washkaji na akiumwa kidogo watu 100 wamepost whatsap status unatembelewa kwa kuletewa juisi na matunda kibao.

Mfano wachezaji wetu wengi walikuwa wakipata team ulaya wanarudi bila sababu za msingi. Wenzetu West Africa mtu akisonga mbele Hakuna kugeuka nyuma.

Mwamba aache kulia kama anavyoitwa machozi hapo Italy kuna vijana wadogo miaka 18-23 kutoka Africa wametulia na watakomaa mpaka mwisho bila kulia lia.

Inaitwa Home Sick ‘Syndrome’.

Wenzetu akitoka ndo imeisha hiyo, atasonga mbele bila kugeuka na sana sana atawavuta na wenzake waende aliko.... sisi tunakumbuka nyumbani na washkaji au familia na kuamua kurudi.
 
Mwambie arudi nyumbani kumenoga ...
Uku dawa imeshapatikana maana Ummy kasema wale wooote wamepimwa wameonekana Positive ..!! (KAMTAJA KWA JINA MGONJWA WA KWANZA TANZANIA)
Sasa sijui positive ndio nini
Ila nimeona wanajipongeza kwa kanzi nzito...!!

Ila Bongo tuko na utoto mwingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msanii wa Tanzania Hussein Machozi anayeishi Italia kwa sasa ambayo ndio nchi iliyoathirika zaidi na Corona ameelezea maisha ya huko ambapo amedai wamefungiwa ndani kwa mwezi mmoja sasa na maisha ni magumu

Msanii huyo amedai pia watu weusi wakiugua ugonjwa huo hawatibiwi kipaumbele wanapewa wazungu kwanza kutokana na huduma za afya kuzidiwa, pia ukiwa na umri wa zaidi ya miaka 40 hutibiwi bali wanapewa kipaumbele vijana

Mwambie arudi home huku mambo ni yente

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona ubaguzi wa rangi hapo nmeona priority kwamba wanapewa vijana wazawa kwahio hata madingi na wamewekwa pembeni wapembeni sasa wewe stranger unalilia wakat umeona hata wazawa pia hawapat hio huduma
 
Inaitwa Home Sick ‘Syndrome’.

Wenzetu akitoka ndo imeisha hiyo, atasonga mbele bila kugeuka na sana sana atawavuta na wenzake waende aliko.... sisi tunakumbuka nyumbani na washkaji au familia na kuamua kurudi.
Kuna jamaa yangu alijilipua na kufanikiwa kuingia Serbia, akapata kazi za part time baada ya miezi 3 karudi Bongo analalamika kule maisha magumu, upweke na amekuja kujipanga vizuri. Kaishia kuja na begi la ngozi, raba na jeans. Chenji alizobakiwa nazo ziliisha ndani ya week.

Alipofika maskani na kutupa habari hizo kila mtu alitaka ampige kofi la uso.

Saizi hata nauli ya kurudi tena imekuwa mbingu na ardhi.
 
Kuna jamaa yangu alijilipua na kufanikiwa kuingia Serbia, akapata kazi za part time baada ya miezi 3 karudi Bongo analalamika kule maisha magumu, upweke na amekuja kujipanga vizuri. Kaishia kuja na begi la ngozi, raba na jeans. Chenji alizobakiwa nazo ziliisha ndani ya week.

Alipofika maskani na kutupa habari hizo kila mtu alitaka ampige kofi la uso.

Saizi hata nauli ya kurudi tena imekuwa mbingu na ardhi.
Watanzania wengi siyo ma-fighter. Kusema kweli tumezoea maisha ya kimkanda mkanda sana. Ukienda nchi zilizoendelea utakuta wahindi wachina wanachakarika na wafrika kutoka West Africa wachakarika vibaya sana na hawalalamiki. Ukija kwa mtanzania kila siku ni kulalamika. Kazi wanasema ni ngumu, mara upweke.... Kulalamika imeshakuwa kama utamaduni wetu.
 
Back
Top Bottom