Msanii alikufa afufuka afrika kusini

3squere

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
925
181
Msanii aliyekufa 'afufuka' Afrika Kusini
6 Februari 2012 23:23
Mtu mmoja nchini Afrika Kusini anayedai kuwa ni mwanamuziki
mashuhuri aliyekufa, anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo hadi
watakapothibitisha utambulisho wake kwa vipimo vya DNA,
wamesema polisi.
Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo -
mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki
mwaka 2009.
Anadanganya
Hata hivyo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita
akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.
Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema
anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema
atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA
vitaonesha anadanganya.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Nomsa Maseko
amesema polisi wanatarajia kupata majibu ya vipimo vya DNA
baadaye wiki hii - na mpaka wakati huo mtu huyo atasalia
kizuizini.
Mashabiki
Mwandishi wetu anasema iwapo vipimo vya DNA vitaonesha
kweli ni Bw Khumalo, polisi watalazimika kwenda mahakamani
kupata kibali cha kufukua maiti, ili kujua nani hasa alizikwa,
katika mazishi yaliyokuwa ya hali ya juu ya Bw Khumalo
ambayo yalihudhuriwa na wanasiasa, vyombo vya habari na
mashabiki wake.
Mwandishi wetu anasema kesi hiyo imezua kizazaa nchini
Afrika Kusini - na siku ya Jumapili iliyopita, maelfu ya mashabiki
walikwenda Kwazulu-Natal kushuhudia "kutolewa" rasmi kwa
mtu huyo.
Polisi walitumia maji yenye nguvu kutawanya watu baada ya
msongamano kutokea kutokana na kila mtu kutaka kumuona
mtu anayejiita Bw Khumalo.
Upelelezi
Akitumia kisemeo, aliwaambia mashabiki wake kuwa hakuwa
amekufa - lakini alipotea baada ya kuchukuliwa na wachawi.
Amesema alifungiwa katika pango na mizimu kwa miaka
miwili, na alilazimishwa kuimba na kulazimika kula matope ili
asife kwa njaa.
"Nimekuwa hai muda wote," amekaririwa akisema na gazeti la
The Times la Afrika Kusini.
"Nimepoteza uzito mwingi lakini ni mimi," alisema.
Mtu huyo, ambaye hakuwa na mtindo wa nywele wa rasta
ambao Bw Khumalo alikuwa nao, alipuuza ombi la mashabiki la
kumtaka aimbe, badala yake alitaja majina ya ukoo wake, kwa
mujibu wa gazeti la The Times.
Polisi wa Afrika Kusini wamesema wanashughulikia mkasa huo
kwa kufanya upelelezi wa kesi ya uhalifu.
Alamisha hii
 
hahahahaah daaah kwakua alikua msanii , huenda aliwasanii juu ya kifo chake.
 
vijimambo hivyo.

Mbona aligoma kuimba ili kudhibitisha kuwa ndio yeye.

Ila kwa taarifa yenu tu. mimi ndio Tupac Shakur. Siri yenu msimwambie m2. Nasubiria siku ya siku niwaibukie kule home kwetu.
 
humu duniani kila siku usanii mpya.... jamaa amegoma kuimba labda mashairi yamepotea kichwani mambo ya usukule
 
MKUU! Jana nilishtuka kusikia kisa hicho. Mwandishi wa BBC alisema huyo Msanii amekuwa anaishi na mke wa msanii aliyekufa....na inasemekana huyo mama amesema ni mjamzito!
Msanii aliyekufa 'afufuka' Afrika Kusini
6 Februari 2012 23:23
Mtu mmoja nchini Afrika Kusini anayedai kuwa ni mwanamuziki
mashuhuri aliyekufa, anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo hadi
watakapothibitisha utambulisho wake kwa vipimo vya DNA,
wamesema polisi.
Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo -
mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki
mwaka 2009.
Anadanganya
Hata hivyo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita
akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.
Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema
anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema
atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA
vitaonesha anadanganya.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Nomsa Maseko
amesema polisi wanatarajia kupata majibu ya vipimo vya DNA
baadaye wiki hii - na mpaka wakati huo mtu huyo atasalia
kizuizini.
Mashabiki
Mwandishi wetu anasema iwapo vipimo vya DNA vitaonesha
kweli ni Bw Khumalo, polisi watalazimika kwenda mahakamani
kupata kibali cha kufukua maiti, ili kujua nani hasa alizikwa,
katika mazishi yaliyokuwa ya hali ya juu ya Bw Khumalo
ambayo yalihudhuriwa na wanasiasa, vyombo vya habari na
mashabiki wake.
Mwandishi wetu anasema kesi hiyo imezua kizazaa nchini
Afrika Kusini - na siku ya Jumapili iliyopita, maelfu ya mashabiki
walikwenda Kwazulu-Natal kushuhudia "kutolewa" rasmi kwa
mtu huyo.
Polisi walitumia maji yenye nguvu kutawanya watu baada ya
msongamano kutokea kutokana na kila mtu kutaka kumuona
mtu anayejiita Bw Khumalo.
Upelelezi
Akitumia kisemeo, aliwaambia mashabiki wake kuwa hakuwa
amekufa - lakini alipotea baada ya kuchukuliwa na wachawi.
Amesema alifungiwa katika pango na mizimu kwa miaka
miwili, na alilazimishwa kuimba na kulazimika kula matope ili
asife kwa njaa.
"Nimekuwa hai muda wote," amekaririwa akisema na gazeti la
The Times la Afrika Kusini.
"Nimepoteza uzito mwingi lakini ni mimi," alisema.
Mtu huyo, ambaye hakuwa na mtindo wa nywele wa rasta
ambao Bw Khumalo alikuwa nao, alipuuza ombi la mashabiki la
kumtaka aimbe, badala yake alitaja majina ya ukoo wake, kwa
mujibu wa gazeti la The Times.
Polisi wa Afrika Kusini wamesema wanashughulikia mkasa huo
kwa kufanya upelelezi wa kesi ya uhalifu.
Alamisha hii
 
Fingerprints zake zimeonesha kuwa hazifanani na za marehemu aliyezikwa. Badala yake imegundulika kuwa ni prints za jambazi hatari lililokuwa linatafutwa.

Ama kweli...jambazi/tapeli limeshamweka mimba mke wa marehemu. Historia ya mtoto atakayezaliwa itakuwa ya kiaina.

Na suala la HIV status yake?...... ni utata.
 
huyu jamaa sanaa kweli ameshampa mjane wa watu kibendi.
halafu mbaya zaidi ndugu wanakomalia ndiye yeye,mwanamke akaingia mkenge.

lakini huyu mwanamke naye kimeo si angemwuliza umri wa watoto wao wakubwa?na akissema amesahau amwulize mbona hakumsahau mwanaike?au hakusahau kuichapa?
 
Back
Top Bottom