Msanii afufuka huko Bondeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msanii afufuka huko Bondeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Msanii afufuka huko Bondeni[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  Picha ya msanii anayedaiwa kufufuka[/TD]
  [TD]
  Shirika la habari la BBC linaliripoti kuwa Mtu mmoja nchini Afrika Kusini anayedai kuwa ni mwanamuziki mashuhuri aliyekufa, anashikiliwa na polisi hadi watakapothibitisha utambulisho wake kwa vipimo vya DNA.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo - mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki mwaka 2009. Hata hivyo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.

  Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA vitaonesha anadanganya.

  Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Nomsa Maseko amesema polisi wanatarajia kupata majibu ya vipimo vya DNA baadaye wiki hii - na mpaka wakati huo mtu huyo atasalia kizuizini. Kesi hiyo imezua kizazaa nchini Afrika Kusini - na siku ya Jumapili iliyopita, maelfu ya mashabiki walikwenda Kwazulu-Natal kushuhudia "kutolewa" rasmi kwa mtu huyo.

  Akitumia kisemeo, aliwaambia mashabiki wake kuwa hakuwa amekufa - lakini alipotea baada ya kuchukuliwa na wachawi. Amesema alifungiwa katika pango na mizimu kwa miaka miwili, na alilazimishwa kuimba na kulazimika kula matope ili asife kwa njaa. "Nimepoteza uzito mwingi lakini ni mimi," alisema. Mtu huyo, alitaja majina ya ukoo wake.

  Polisi wa Afrika Kusini wamesema wanashughulikia mkasa huo kwa kufanya upelelezi wa kesi ya uhalifu.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mbona unaguna? hauamini?:lol:
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wewe umeamini?

  isije kuwa alifichwa na 'nyumba ndogo'? think RR think...
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hahahahaha,
  The police is testing his DNA because the death is/was certain, what is not certain is the identity of this new person...
  So he died and was probably buried.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  so kafufuka???
   
 7. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwangu mimi naona it is an impostor
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  he he hee kaja ku rithi mali na wake za jamaa?lol
   
 9. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndio hivo.
  watu walikua wanamwambia: mbona unamfanana yule msanii alie fariki?
  then he decided to learn his history, his songs, his body language etc. it took 2 years.
  Now he is back. Watu wamechanganyikiwa kwa furaha, they wish it is true (hasa wake zake)
  But let the DNA test take place kwanza.
   
 10. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he,the boss u r right inawezekana jamaa aliwekwa ndani na nyumba ndogo
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Jamani msisahau huyo jamaa ni msanii,labda kuna usanii aliufanya
   
 12. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  A man who claimed to be a famous dead singer has been charged with fraud, South African police say.
  [​IMG]
  The man said he was Khulekani "Mgqumeni" Khumalo - an award-winning Zulu folk musician who died in 2009.

  He claims he was kidnapped by a witchdoctor who cast a spell on him and held him in a cave with zombies, local media reported.

  But police say the man's fingerprints establish that he is in fact Sibusiso John Gcabashe, 28.

  Khumalo's apparent return from the dead had sparked frenzied scenes as fans flocked to the singer's family home at the weekend, with riot police deploying truncheons and water cannon to control them.

  The apparent impersonator appeared at Nquthu magistrate court in KwaZulu-Natal on Tuesday where he was charged with fraud but not asked to enter a plea, said police spokesman Col Jay Naicker.

  He has been remanded in custody until 14 February when his bail application - which the state is expected to oppose - will be heard.

  'Hooligan'
  Family of the dead singer appeared split over the man's identity, with two wives saying he was genuine but the singer's former partner, Zehlise Xulu, insisting he was not.

  Ms Xulu, who has a 10-year-old son by Khumalo, said she hoped the man would be convicted and sent to jail for a long time for "bringing back old pains".

  "My son travelled all the way from Johannesburg with the hope of seeing his father, only to find that the man was a hooligan," she said according to The Mercury newspaper.

  "I was annoyed when he repeatedly referred to me as his lover," she said.

  Belief in witchcraft is common in South Africa, especially in rural areas
   
 13. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Akaah! watu wamesha mlilia mpaka wameshukuru mungu halafu anakuja hadith zake za Abunuasi.
   
 14. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Hata mimi mshkaji wangu mmoja alikufa katika mazingira ya kutatanisha lakini kuna dada mmoja mara nyingi alikuwa ananipigia simu na kuniuliza kama jamaa kahamia kimara coz kila siku asubuhi walikuwa wanakutana stendi,mimi nikimwambia amekufa haamini mpaka siku nilipo mkutanisha huyo dada na familia ya huyo mshkaji,hata hapa mtaani watu wengi walikuwa wanamuona hadi ndugu zake wakaamua kuleta waganga ili jamaa asiwatokee tena watu.Dunia ina mambooooooo!!!!!
   
 15. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  vichwa vya waafrika wengi vina waza maswala ya ushirikina tu
   
 16. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  mSUKULE ATABAKI KUWA MSUKULE!!
   
 17. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimependa jinsi police wa south walivo react. Hapa Bongo huyo bwana angepelekwa nyumba za ibada kuombewa. Wacha wakampime wambaini ili wamtie ndani na usanii wake.kiboko ya uchawi ni sayansi. He wont cheat the DNA test.
   
Loading...