superfisadi
JF-Expert Member
- May 22, 2009
- 553
- 54
Msando amburuza kortini Mwanasheria Mkuu wa serikali
na Grace Macha, Moshi
DIWANI wa kata ya Mabogini, Albert Msando (CHADEMA), amemfikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi akipinga taratibu zilizotumika kumchagua mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Kesi hiyo namba moja ya mwaka 2011 ilifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Moshi, Simon Kobelo, ambapo diwani huyo anapinga utaratibu uliotumika wakati wa mkutano wa halmashauri hiyo uliofanyika Desemba 17, 2010 aliodai ulikiuka sheria na kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi.
Msando ambaye ni wakili machachari wa kujitegemea alidai kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria kwani madiwani waliapishwa na mwanasheria wa halmashauri badala ya hakimu mkazi au wa wilaya inavyotakiwa kisheri.
Aliieleza mahakama hiyo kuwa dosari nyingine katika uchaguzi huo ni kitendo cha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Anna Mwahalende, kujiteua kuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wakati sheria inataka madiwani kumchagua mwenyekiti wa muda miongoni mwao ili aendeshe zoezi la uchaguzi.
Hivyo aliiomba mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ili kuruhusu madiwani wa halmashauri hiyo kuapishwa na hakimu mkazi pamoja na uchaguzi huo kurudiwa. Kwa upande wake wakili wa serikali, Abdalah Chavulla, aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kisheria akipinga madai hayo na kuiomba mahakama hiyo kuisikiliza kesi ya msingi kwa njia ya maandishi jambo ambalo lilipingwa na diwani Msando ambapo hakimu Kobelo alikubali pingamizi hilo hivyo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa njia ya kuongea jambo ambalo litasaidia kupunguza muda wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Katika uchaguzi huo diwani wa kata ya Okaoni, Moris Makoye (CCM), alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Meja Jesse Makundi wa TLP alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti ambapo Msando alikuwa ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia CHADEMA.
My take
kumbe wanajf ni wabishi mpaka uraiani?:msela: