Msamaha!

God bell

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2011
Posts
590
Reaction score
211
Ndugu wana MMU nawasalimuni wote, poleni kwa majukumu. Nakuja na ujumbe huu jioni hii. Nawaombeni msamaha wale wote nilowakosea aidha kuwaudhi au kwa kukwaruzana katika nyuzi mbalimbali nilipokuwa nachangia au Kupeana ahadi katika PM ambazo baadae hazikuzaa mafanikio. Kuna kipindi nilimjibu mtu hapa baada ya kuniudhi nikamjibu vibaya akanisababishia BAN. Wote hao nawaomba msamaha. Ni hayo tu ili niweze kutua mzigo kwenye roho yangu níishi kiroho safi. Asanteni. Mwenye maoni anakaribishwa.
 
Nimekusamehe siku nyingine usinidanganye utanioa Jf af usinioe....
 
Uache hasira hata kwa watu usiowafahamu wala kuwaona. Halafu ulipe lile deni la watu usiishie tu kuomba msamaha!
 
wengine hatujui hata ulifanyaje..................


kuwa na amani ndugu.....
 
Sio yule jamaa Mpiga msuli amechange ID anaomba msamaha
 
Umesamehewa eh!be happy,sambaza mapendo humu ndani,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…