Msamaha wa wafungwa-babu seya asahaulika tena. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha wa wafungwa-babu seya asahaulika tena.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by spencer, Dec 10, 2010.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Msamaha wa Rais wawapita kando mafisadi, ‘mafataki’ Send to a friend Thursday, 09 December 2010 21:04 0diggsdigg


  [​IMG] Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mallim Seif Shariff Hamad, wakati wa sherehe za miaka 49 ya Uhuru kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mohamed Gharib Bilal na kulia ni Rais Mstaafu awamu wa tatu Benjamin Mkapa.

  Exuper Kachenje
  RAIS Jakaya Kikwete amewatosa mafisadi na waliowakatisha masomo wanafunzi kwa kuwapa mimba kwenye msamaha alioutoa jana kwa wafungwa 3,563 kusherekea miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
  Taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha imeeleza msamaha wa wafungwa 3,563 uliotolewa na Rasi Jakaya Kikwete wakati wa sherehe za Uhuru mwaka huu hawahusu wafungwa wa makosa ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, hawahusiki na msamaha huo.

  Taarifa hiyo imetaja wafungwa wengine wasiohusika na msamaha huo kuwa ni wafungwa waliowapa mimba wanafunzi na kuwakatisha masomo, waliohukumiwa kunyongwa na waliojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

  Wengine ni wale waliohukumiwa kifungo cha maisha, waliofungwa kwa makosa ya ujambazi, wizi wa magari na waliofungwa kwa kunajisi, kubaka na kulawiti.

  Msamaha huo pia hauwahusu watu wanaotumikia kifungo cha pili au zaidi, wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi za Parole ya mwaka 1994 na Sheria ya huduma kwa jamii ya mwaka 2002.

  "Wafungwa wengine ambao hawamo kwenye msamaha huo ni waliozuia watoto kupata masomo, waliowahi kutoroka chini ya ulinzi, waliohukumiwa kwa makosa ya uharibifu wa miundombinu kama wizi wa nyaya za simu, umeme, njia za reli na transfoma na wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo kwa msamaha wa Rais na bado wanaendelea na kifungo kilichobaki," imeeleza taarifa hiyo.

  Rais Kikwete ametoa msamaha huo akitumia Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka kusamehe wafungwa siku za sherehe za Kitaifa ambazo ni Uhuru na Muungano.

  Tanzania Bara ilipata Uhuru wake kutoka kwa Mwingereza Desemba9, 1961.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya waziri Nahodha, wafungwa wanaonufaika na msamaha huo ni wale wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na ambao hadi jana walishatumia robo ya vifungo vyao na wafungwa ambao ni wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu, saratani ambao wanaoelekea siku za mwisho wa maisha yao na wazee wa zaidi wenye umri wa zaidi ya miaka 70.

  Hata hivyo wafungwa hao watatakiwa kuthibitishwa na jopo la madaktari chini ya mganga mkuu wa mkoa au wilaya.

  Taarifa hiyo imetaja wafungwa watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wanawake waliofungwa wakiwa wajawazito, walioingia magerezani wakiwa na watoto wachanga wanaonyonya na wenye ulemavu wa mwili na akili ambao ulemavu wao utathibitishwa na mganga mkuu wa mkoa au wilaya.

  “Ni mategemeo yetu kwamba watakaoachiwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee gerezani,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya serikali.


  Source:Mwananchi
  :target:
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Babu Seya na Papii haki yao wataipata Mahakama ya Rufaa punde tu itakapopitia tena marejeo waliyoyaoomba...........walionewa vibaya mno....................sababu zilezile zilizotumiwa kuwasafisha watuhumiwa wengine zilipaswa kutumika kuwaachilia huru wao...............
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Hivi yule aliyekuwa anawapeleka kwa babu Seya wale watoto alichukuliwa hatua gani? Kuna ajuaye anijuze????:focus:
   
 4. B

  Bongemzito Senior Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anatesa town
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Papaa Liyumba naye vipi! Maana mjini hapatatosha!
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  QUOTE=spencer; kusherekea miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


  Si kweli. Hakuna nchi inayoitwa Tanzania Bara ambayo ilipata uhuru siku hiyo. Huyo mwandishi Kachenje sijui hasipotoshe historia. Historia inasema siku hiyo nchi ya Tanganyika ndiyo iliyopata uhuru (ingawa wa bendera).
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Penye nyekundu, ndipo hasa iliposababu ya kwanini Babu seya hajaachiwa na wala usitegemee kupewa msamaha wa Rais. kutoka kwake ni kushinda kesi dhidi yake katika rufaa aliyoikata.
   
Loading...