Msalato, Mzumbe, Tabora Boys, Minaki na nyingine za vipaji maalum ziko wapi?

Msulunje

Member
Oct 6, 2015
67
35
Kati ya shule kumi bora kwa matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka hivi punde, hakuna hata shule moja ya serikali imepenya. Ziko wapi Ilboru, Mzumbe, Tabora Boys, Msalato Girls, Kilakala na nyinginezo nyingi? Je, kuna haja ya kubinafsisha shule za umma pia?

Leo ni mtoto wa kiongozi gani wa ngazi ya juu serikalini anasoma Tabora Boys, Bwiru, Kilakala, Msalato n.k.? Shule za umma zinapaswa kuungwa mkono sana hasa na watu wanaoongoza nchi na kufanya maamuzi!

Si ajabu tunashangaa kuwa mke wa Rais JK, Bi. Salma- alikuwa mwalimu wa shule ya serikali lakini huwenda watoto wa JK wa hivi karibuni hawakuwahi kusoma shule za serikali (Achilia kina Ridhiwani Kikwete ambao walisoma enzi za shule za umma). Huwenda pia, mke wa JPM, Bi. Janeth Magufuli ambaye ni mwalimu - watoto wake (ambao ni watoto wa rais) hawasomi kwenye shule za serikali.

Huwenda pia watoto wa mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na hata wakuu wa shule za serikali wenyewe (watoto wao) hawasomi kwenye shule za serikali.

Na sijamuuliza dada yangu Bi. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu wa sasa - watoto wake wanasoma shule zipi. Najua waziri aliyeondoka, Shukuru Kawambwa - watoto wake walikuwa wanasoma "INTANESHNOZ"!

Hapa pana jipu la kutumbua! Tuko tayari wake zetu na waume zetu wawe walimu kwenye shule za serikali lakini hatuko tayari watoto wetu wasome kwenye shule za serikali kwa sababu tunajua shule hizo zitaua ndoto na matumaini yao kupata elimu bora!

Natamani kama alivyopiga marufuku SUKARI kutoka nje, pia apige marufuku viongozi wa umma wa ngazi za maamuzi ya nchi kusomesha watoto kwenye INTANESHNOZ! Ikitokea hivyo, sote tutaona namna shule za umma zinavyoboreshwa kwani watajua wakicheza nazo hata watoto wao wataathirika milele.

Lakini watoto wa watunga sera na wafanyaa maamuzi wakiendelea kusoma INTANESHINOZ! Shule za umma na elimu bure vitakuwa "bure kweli"!
 
Usisahau jambo muhimu sana, hao unaowasema ndio wamiliki wa hizo shule za kimataifa na Kiwanji medium, au Kihaya medium. Moja iko njiani inaingia sokoni, inajengwa pale mbele ya Chalinze njia ya Morogoro mkono wa kulia.

Hakuna kitu cha bure chini ya jua mkuu.
 
Nimeaumia sana Tabora boys kuwa ya 123.Magufuli na mama Ndalichako okoweni shule za uma ndio kimbilio la walio wengi?.
 
Wala kuzirejesha hawawezi approach inagoma unless waendeshe kibiashara. Fedha ndo equilibrium point these days huduma is too good to be an assert in fact it is relative concept. Hela baba hela ndo habari zq capitalists ambao wenye vipaji wore wanatumika huko.
 
Nimeshangaa sana.....na kwa uhakika Magufuli anaiua kabisa elimu ..hasa shule za kata ,ndio hakuna michango ,ila hata wale walim wa kujitolea kuwapa angalau maarifa wanafunzi hasa kwenye masomo ya sayans hawapo ,pili chakula shuleni hakuna wakati watoto wa shule za binafsi wanakula vizuri huku serekalini ,hakuna chakula kwa zuio la serekali kuwa wazaz wasichangishwe ...huu ni uonevu na kuwanyanyasa wa toto wa maskin ...ndo maana watazid kufeli mitihani
 
shule hizi zibinafsishwe tu hata zile za kata ili ziendeshwe kwa ufanisi
 
jaman aliyeharibu elimu yetu na kuweka record ni yule waziri aliyeunganisha masomo aka mzee wa group subject. Physics,Chemistry & Bio kua somo moja nk nk. tusimsahau
 
Back
Top Bottom