Msala ambao siwezi usahau kamwe

Mimi wakati chaliii nilikua mtundu mtundu...nikikua na michezo ya ajabu ajabu ya mitego ambayo nilikua naifanya kwa wenzangu...siku moja nilimuumiza mtoto wa jirani...jirani akasubiri wazee hawapo..maana kwa kipindi hicho mm nilikua naingia shuke mchana (standard 1).
Siku ikafika nashangaa mlango unagongwa (nilikua peke yangu)...nilipoenda kufungua mlango tu hamadi maza wa mtoto niliyemuumiza huyu hapa (alikua anaitwa mama Tizo)..maza alikua amebeba kifurushi cha stiki...asee nilichezea sana stiki hiyo siku hadi nilishindwankwenda shule.
Jioni wazee wamerudi nikawasimulia...coz walishangaa wamenikuta nmelala badala ya kuwa shule...nikipowasimulia mzee akapandwa na hasira akamfuata huyo maza...nahisi mwisho wa siku waliyasuluhisha kuutuuzima..Baada ya kesi kuiisha yule maza alihama ule mtaa sijui tatizo likikua ni nini...Tangu hapo utundu utundu wangu ukapungua.
 
Kweli we mcheza viduku [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kweli huu ulikuwa msala.Lazima ulipungua kilo kadhaaa
Mitihani vipi? Ulibutua?
 
Kweli huu ulikuwa msala.Lazima ulipungua kilo kadhaaa
Mitihani vipi? Ulibutua?
Nilipata Wastani, Necta ndio nikafanya kweli, na ule msala ulichangia mimi kufaulu, maana niliacha upuuzi wote nikawekeza nguvu..
 
interesting mi mtoto wangu mtundu sana siku nataka niende shuleni kwao wanisimulie vituko vyake manake juzi kaja kapoteza begi na kila kitu
 
Niliiba dawa ya mtoto (mdogo wangu) hizi syrup tamu za watoto, nikaimimina kwenye glass, nikakatakata vipande vya viazi nikaweka mezani najifanya padre naongoza ibada,
ile syrup nimefanya ndio divai na vile vipande vya viazi ndio mkate, wadogo zangu ndio waumini [emoji23][emoji23] Kipigo nilichokipata siku hiyo sitakisahau,
 
Unapata nini ukidanganya?
 
Duh
 
Shule tuliambiwa Carbondioxide inazima moto, nikawaza zile dawa za kupuliza zinauaje wadudu nikajifikirisha nikasema itakuwa pia ina Carbondioxide hivyo ukiwapulizia inawazima pia, basi buana nikarudi home nikachukua utambi wa jiko la mchina ulioisha jikon nikautia kiberiti unawaka sawa sawa, nikaenda chumbani kuchukua dawa ya kupulizia enzi zile rungu ndio inaanza anza, nikaja kupulizia kwenye moto ili uzime, kilichotokea sasa..........
 
Dah umenikumbusha mbali,home kulikuwa na kwamba za chuma za kuanikia nguo kuna siku Mama alinifunga juu kama nguo alinichapa vibaya sana.dah hawa Wazazi wa zamani walikuwa nuksi sana.
 
Huna maana kabisa..,..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
 
Ole mbole gete....
 
Mkuu story yako ni kama ya juma na uledi. Miaka ya 2020+ unazungumzia mwaka huu. Hiyo miaka 15 badae bado haijafika.

Hii story yako mkuu, hapana
 
maneno tunaysubri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…