Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Kwa miezi kadhaa sasa, picha na video kutoka Jamhuri ya Dominika zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, zikionesha maafisa usalama, polisi na wanajeshi wakiendesha misako ya barabarani, wakikamata watu wanaoshukiwa kuwa wahamiaji haramu – wengi wao wakiwa ni kutoka taifa la Haiti.
Hii ni kampeni rasmi ya serikali ya Dominika dhidi ya uhamiaji haramu, hasa kutoka taifa jirani la Haiti. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamlaka za ndani, zaidi ya wahamiaji 250,000 walifukuzwa nchini humo mwaka 2024 pekee.
Rais Luis Abinader alitangaza lengo la kufukuza wahamiaji 10,000 kila wiki, hatua iliyoelezwa kuwa ni "kupunguza mzigo wa kijamii na kiuchumi unaosababishwa na uhamiaji haramu huku akitaka hali ya kiusalama ndani ya Dominika kuendelea kuimarika".
Misako hiyo inajumuisha ukaguzi wa magari, kusimamisha mabasi na kupekuliwa kwa abiria, pamoja na uvamizi wa nyumba usiku. Watu wanaokamatwa hupelekwa kwenye vituo vya mahabusu kabla ya kufukuzwa kutoka Dominika.
Mashirika ya haki za binadamu, kama vile Amnesty International na Human Rights Watch, yameonya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, huku baadhi ya waliokamatwa wakiripoti kupigwa, kina mama wajawazito kudhalilishwa na kutengwa kwa misingi ya rangi au lugha.
Tangu enzi katika historia, uhusiano kati ya Haiti na Jamhuri ya Dominika umekuwa wa mivutano na sitofahamu. Wahaiti wamekuwa wakihusishwa na kazi ngumu na duni kama vile ukulima wa miwa, lakini mara nyingi hukumbwa na chuki na ubaguzi katika jamii ya Kihispania ya Dominika.
“Border of Lights: The Haitian-Dominican Divide” ni kitabu ambacho kimeandikwa na bi mdada Edwidge Danticat, ndani yake kinachambua uhasama wa kihistoria kati ya mataifa hayo mawili.
Danticat kwa mara nyingine alionesha wasiwasi wake katika mgogoro baina ya nchi hizi mbili, huku akonesha watu maelfu kutoka Haiti kupoteza maisha ndani ya nchi ya Dominika. The Farming of Bones sio kitabu cha mtu mwenye roho nyepesi kwani kinatoa machozi haswa, humo ndani kitabu hiki kinaeleza kwa undani jinsi tofauti za kitaifa na kikabila zilivyochangia machafuko na vifo vya maelfu.
Kuona raia wa Haiti kukimbia Haiti na kuingia Dominika sio kosa kwa jicho la haki za binadamu, nitafafanua kidogo upate kunielewa:
Mtandao wa Insightcrime imeielezea dunia kuwa Haiti kama nchi zingine, Brazil, Colombia pamoja na Ecuador, kuna kundi moja la uhalifu kwa jina la G9 Family ambalo linaongozwa na Jimmy Cherizier maarufu kwa jina la Barbecue, ndani ya kundi hili kuna mangenge zaidi ya tisa mojawapo likiwa ni Delmas 6, pamoja na Baz Pilate ambalo hili linaunda na waliokuwa askari wa kitengo cha SWAT walioacha kazi. Kitaalamu ni unakutana na watu waliopata elimu na utaalamu wa matumizi ya silaha, Special Weapons And Tactics.
Ebu vuta picha unakutana na vijana watano wakiwa na silaha tena waliopitia mafunzo ya SWAT, je kuna kupona hapo? hawa jamaa wamepata mafunzo mpaka ya kijeshi sasa wamebadilisha gear juu kwa juu, G9 Family linafanya mambo yake kwenye maeneo yanayozunguka maeneo ya Port-au-Prince.
Ukiachana na hawa, kuna majanja wanaitwa 400 Mawozo sio Mawazo bali ni Mawozo ila hawa madogo janja wanafanya vitendo vinavyowapa mawazo haswa wakazi wa maeneo ya Ganthier na baadhi ya maeneo ya Port-au-Prince. Kiongozi wa 400 Mawozo ni janja mmoja bingwa kwa jina la Wilson Joseph maarufu kwa jina la Lanmo Sanjou. kwa ujumla ndani ya Haiti kuna mangenge ya uhalifu zaidi ya 100 huku mangenge mengi yakiwa ndani ya Port-au-Prince.
Mangenge haya yanahusika na utekaji, mauaji, uuzaji wa madawa ya kulevya, silaha nzito, huku yale mangenge makubwa kama yaliyopo ndani ya G9 Family wakienda mbali zaidi ya kusimamia uendeshaji huduma za kijamii kama utoaji wa umeme, maji pamoja na kusimamia usafirishaji katika barabara za mitaa ambayo wanaiongoza.
Mwezi wa tano mwaka huu, Bibiye Kristi Noem ambaye ndio anaiongoza idara ya Department of Homeland Security imeainisha kuwa mangenge mawili ya Viv Ansanm pamoja na lile la Gran Grif ni makundi ya kigaidi kwani haya mangenge mawili yanamiliki zaidi ya 85% ya mji wa Port-au-Prince na yamekuwa yakihusika na utekaji pamoja na mauaji.
William O'Neill kapewa kazi ngumu sana ya kutazama hali ya usalama ndani ya Haiti, na baraza la UN kutazama hali ya usalama na Haki za binadamu ndani ya Haiti. Kazi ambayo amepewa ni ngumu ingawa aliweza kufanya kazi zingine zenye ufanano huo.
O'Neill amewahi kuwa Chief of the UN Human Rights Field Operation ndani ya Rwanda, mwaka 1995 alisaidia kwa kiasi kikubwa kuweka miongozo bora ya kurekebisha jeshi la polisi la Haiti, O'Neill amefanya kazi ndani ya nchi zaidi ya 10 ila shughuli ambayo amekutana nayo ndani ya Haiti ni funga kazi.
Nilipata nafasi ya kutembelea maktaba moja hapa Dar es Salaam na kusoma kitabu cha “Haiti: The Tumultuous History” kilichoandikwa na na Philippe Girard, kitabu hiki kinaeleza hali ya kisiasa na kiuchumi inayowasukuma wahaiti kutafuta maisha bora nje ya nchi yao na wengi kujikuta wakiingia Jamhuri ya Dominika kukimbika mangenge.