Kwa hiyo unamuona msajili wa vyama vya siasa hana role kwenye uchaguzi?!
Ha ha ha...Nguvu ya polisi ni swala muhimu katika kukabiliana na maandamano yasiyo na kibali.
Kumbuka msajili wa vyama alitoa tamko na maelekezo ya vyama kuhakikisha mawakala wana sifa zote siku saba kabla ya uchaguzi...yaani aliwakumbushia kwa nia njema kwani asingetakiwa kufanya hivyo kwa kuwa liko wazi kiutaratibu.
Msajili wa vyama vya siasa nchini awaibukia chadema
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018
Akizungumza na Mwananchi leo Februari 22, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.
Jaji Mutungi alipoulizwa kuhusu hilo amesema hawezi kusema lolote kwani yeye anawasiliana moja kwa moja na vyama vya siasa na si vyombo vya habari.
Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.
Chanzo: Mwananchi[/
Jaji Mutungi nakumbuka neno lako ulilonena wakati tupo kwenye lift pale jengo la posta tukielekea kwenye ofisi za tume ya uchaguzi miaka imepita sasa, kwa mantiki ya barua yako kwa chadema naelewa nini kilichomo ndani ya moyo wako sina haja ya kufafanua zaidi.
Aliyemtuma hana tatizo na huyo aliyesababisha cdm wakaamua kuandamana maana walikuwa wanatekeleza adhima yake ya kuua upinzani. Huyo aliyemtuma msajlli aiandikie barua anataka kuhakikisha cdm haindelei kufanya siasa hapa nchini na hata ikibidi ifutwe, kwani ni hatari kwa chama chake, na kwa mazingira yalivyo chama chake hakiwezi tena kupambana na cdm kisiasa. Hivyo njia pekee ni hii ya kutumia vyombo vya kimlaka kutekeleza dhamira yake.
Mkuu upinzani madhubuti na makini una sifa gani?
Je upinzani unaopanga mikakati ya kuharibu uchaguzi ndio upinzani madhubuti na makini?
je upinzani unaokiuka kwa makusudi taratibu na sheria zilizoweka ndio upinzani madhubuti na makini?
Je ilikuwa sahihi kwa Chadema kufanya maandamano nje ya muda uliopangwa tena bila kibali?
Unadhani wakati sheria hizi zinawekwa wataalamu walikuwa hawajui tabia chafu kama hizi za Chadema zitatokea?
Wajua sababu ya Civil War ni Watawala Wapumbavu na Waonevu ndio jibuHoja ni kwamba Chadema walipokosa accreditation ya mawakala wao hawakuwa na option yoyote zaidi ya kuvunja sheria?
Je hakukuwa na option ndani ya Sheria wakati na baada ya uchaguzi.??
Mbona Maandamano ya CUF waliyoyafanya baada ya muda wa kampeni tena bila kibari hayakuwa tatizo???? CDM wamekuwa na utaratibu wa kusindikiza wagombea wao tangu siku ya kwanza ya kampeni na haikuwahi kuwa tatizo kwa yeyote.Acha kupanic mkuu!
Nimekuuliza swali muhimu sana kwa manufaa ya Tanzania...usikurupuke kulijibu ,tulia na utafakari na ukishindwa kujibu kalale halafu ujibu kesho.
CHADEMA inajitanabaisha kuwa ni chama mbadala cha kufanya mema na mazuri nchi zaidi ya CCM.
Chadema inapotaka kuingia kwenye madaraka kwa njia za kihuni na ukiukwaji wa sheria sio jambo sahihi na ni bora mara 10000 kuwa na CCM inayovunja Sheria kuliko kuwapa nchi Chadema halafu wafanye mambo yote unayohisi ni mabaya.
SHeria ya uchaguzi na vyama vya siasa au iwe sheria kwa ujumla wake haikubali maandamano bila kibali au kampeni nje ya muda uliotajwa...viongozi wa Chadema wanavyoamua kwa makusudi kukiuka sheria hata kama ni mbaya inaasharia kuwa CHADEMA inajiaandaa kukiuka Sheria hata pale wananchi watakapoipa fursa.
Nikuulize swali tu je CCM ndio ingeamua kuandamana na Polisi wakawaacha waandamane nje ya muda Chadema ingeona ni sawa tu?
Kwa nini Chadema ikiuke sheria ili kubadilisha mambo?
Chadema inalo la kuamua...kama wanaamua kuwa wavunja sheria au waasi basi ijulikane hivyo na wafanyiwe ubaya kama waasi na kama imeamua kuwa ni wafuata demokrasia hawatakiwi hata chembe kukiuka misingi ya demokrasia.
FUTA LICHAMA LA WAHUNI
Vitu vingine vinavyotokea asa hiv upe moyo wako furaha kidogo hebu cheka tuuuh hahahahahhaah...
Maana waeza jikuta wapunguza siku za kuishi bure
Itaje iyo option unayo dhani ingekuwa nzr kwao kuchukua kwa wakati huo, ili ujibiwe vzr.Hoja ni kwamba Chadema walipokosa accreditation ya mawakala wao hawakuwa na option yoyote zaidi ya kuvunja sheria?
Je hakukuwa na option ndani ya Sheria wakati na baada ya uchaguzi.??
Nia ya viongozi wa chadema walokuwepo mkutanoni mbowe included; ... ktk suala la kudai hizo hati ilikuwa njema kabisa ... tatizo ni pale ALIPOTOA KAULI ZA KUCHOCHEA wanachama wa CDM na ksha kwa pamoja kuingia barabarani ....hili ni jambo zuri; lakini asiishe hapo vile vile aandike barua kuulizia kwanini mawakala wa CHADEMA hawakupatiwa hati zao hadi dakika za majeruhi. Haya mambo mengine yanaudhi tu. Maana inalazimisha kuhoji kama CDM wasingefanya maandamano (ambayo kwa kweli yalikuwa nje ya muda na sidhani kama yalikuwa na kibali) na yule binti asingeuawa, kweli CDM wangepata lini accreditation ya mawakala wao?