Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi awalima barua CHADEMA kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Msajili wa vyama vya siasa nchini awaibukia chadema

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 22, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.

Jaji Mutungi alipoulizwa kuhusu hilo amesema hawezi kusema lolote kwani yeye anawasiliana moja kwa moja na vyama vya siasa na si vyombo vya habari.

Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.

Chanzo: Mwananchi

Habari zaido soma=>CHADEMA wamlima barua Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji F. Mtungi
 
hili ni jambo zuri; lakini asiishe hapo vile vile aandike barua kuulizia kwanini mawakala wa CHADEMA hawakupatiwa hati zao hadi dakika za majeruhi. Haya mambo mengine yanaudhi tu. Maana inalazimisha kuhoji kama CDM wasingefanya maandamano (ambayo kwa kweli yalikuwa nje ya muda na sidhani kama yalikuwa na kibali) na yule binti asingeuawa, kweli CDM wangepata lini accreditation ya mawakala wao?
 
Huyo Jaji anatumika na tunajua nia yake ni kutaka kuifutia usajili Chadema

Lakini na sisi tunapaswa kumuuliza,hivi Chadema walifanya maandamano bila sababu yoyote ile??

Hivi kama Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni asingevichelewesha vile viapo vya mawakala wao, hivi kweli Chadema wangeweza kuandamana??

Wanachofanya hao CCM ni "kuiprovoke" Chadema ili baadaye waitafutie kesi!
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini jaji mutungi ameiandikia barua chadema akidai kwanini asiichukulie hatua za kisheria dhidi ya maandamano walioyafanya tarehe

16/02/2018,kinyume na utaratibu. maandano hayo yalipelekea kuuwawa kwa mwanafunzi wa NIT ,marehemu Akwilina

Tayari barua hiyo imopokelewa na mkurugenzi wa mawasiliano sera na mambo ya nje wa chadema ndugu John Mrema .

Majibu ya barua hiyo yanatakiwa yajibiwe kabla ya tarehe 25/02/2018
 
hili ni jambo zuri; lakini asiishe hapo vile vile aandike barua kuulizia kwanini mawakala wa CHADEMA hawakupatiwa hati zao hadi dakika za majeruhi. Haya mambo mengine yanaudhi tu. Maana inalazimisha kuhoji kama CDM wasingefanya maandamano (ambayo kwa kweli yalikuwa nje ya muda na sidhani kama yalikuwa na kibali) na yule binti asingeuawa, kweli CDM wangepata lini accreditation ya mawakala wao?
Hoja ni kwamba Chadema walipokosa accreditation ya mawakala wao hawakuwa na option yoyote zaidi ya kuvunja sheria?
Je hakukuwa na option ndani ya Sheria wakati na baada ya uchaguzi.??
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini jaji mutungi ameiandikia barua chadema akidai kwanini asiichukulie hatua za kisheria dhidi ya maandamano walioyafanya tarehe 16/02/2018,kinyume na utaratibu. maandano hayo yalipelekea kuuwawa kwa mwanafunzi wa NIT ,marehemu Akwilina
Tayari barua hiyo imopokelewa na mkurugenzi wa mawasiliano sera na mambo ya nje wa chadema ndugu John Mrema .
Majibu ya barua hiyo yanatakiwa yajibiwe kabla ya tarehe 25/02/2018

Sio kuilima barua tu, akiweza aifute kabisa maana cdm imedhihirika ni tishio kubwa kwa ccm. Na kwabahati mbaya ccm haiwezi tena kushindana na cdm kisiasa zaidi ya kumwaga damu za watu ili ccm isalie madarakani.
 
Eti kinyume na utaratibu??? Kwa nini asiandike kinyume cha katiba?? Hawa nao ni mateka.
 
Mkurugenzi wa uchaguzi naye anastahili apate yake pia
 
Huyo Jaji anatumika na tunajua nia yake ni kutaka kuifutia usajili Chadema

Lakini na sisi tunapaswa kumuuliza,hivi Chadema walifanya maandamano bila sababu yoyote ile??

Hivi kama Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni asingevichelewesha vile viapo vya mawakala wao, hivi kweli Chadema wangeweza kuandamana??

Wanachofanya hao CCM ni "kuiprovoke" Chadema ili baadaye waitafutie kesi!

chadema walifanya maandamano bila ya kibali, hili ndiyo kosa KUU, hayo mengine yote mtajijua!
 
hili ni jambo zuri; lakini asiishe hapo vile vile aandike barua kuulizia kwanini mawakala wa CHADEMA hawakupatiwa hati zao hadi dakika za majeruhi. Haya mambo mengine yanaudhi tu. Maana inalazimisha kuhoji kama CDM wasingefanya maandamano (ambayo kwa kweli yalikuwa nje ya muda na sidhani kama yalikuwa na kibali) na yule binti asingeuawa, kweli CDM wangepata lini accreditation ya mawakala wao?
Mkuu wewe siyo mgeni wa siasa za nchi hii, hilo hawezi kuuliza hata kwa bahati mbaya. Anajua vema kwanini CDM hawakupatiwa hati zao mapema.
 
hili ni jambo zuri; lakini asiishe hapo vile vile aandike barua kuulizia kwanini mawakala wa CHADEMA hawakupatiwa hati zao hadi dakika za majeruhi. Haya mambo mengine yanaudhi tu. Maana inalazimisha kuhoji kama CDM wasingefanya maandamano (ambayo kwa kweli yalikuwa nje ya muda na sidhani kama yalikuwa na kibali) na yule binti asingeuawa, kweli CDM wangepata lini accreditation ya mawakala wao?

Aliyemtuma hana tatizo na huyo aliyesababisha cdm wakaamua kuandamana maana walikuwa wanatekeleza adhima yake ya kuua upinzani. Huyo aliyemtuma msajlli aiandikie barua anataka kuhakikisha cdm haindelei kufanya siasa hapa nchini na hata ikibidi ifutwe, kwani ni hatari kwa chama chake, na kwa mazingira yalivyo chama chake hakiwezi tena kupambana na cdm kisiasa. Hivyo njia pekee ni hii ya kutumia vyombo vya kimlaka kutekeleza dhamira yake.
 
Back
Top Bottom