Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,228
- 13,450
Anatumia madawa gan huyo dogo?
kuna hospital special kwa ajil ya victims wa drugs au rehabs.
but kabla hamjafikiria kumpeleka kwenye matibabu ingefaa mkae nae na muongee nae kwa kirefu. Kujua ni kwanin alianza kutumia madawa pia mjue kama anajutia kuacha shule na kupoteza future yake.
pia mumpe mifano ya marafik zake wa utotoni wenye mafanikio mazuri shuleni. Cha msingi mnatakiwa muongeenae kwa upole na upendo huku mukimtengenezea mazingira ya ku regret tabia yake ya kutumia madawa.
akisha regret atakuwa tayar kuacha na hapo ndo mumpeleke rehabs au hospital kwa matibabu,uangalizi na ushauri zaid.
Mkuu hakuna mvuta unga aliekolea ambae aliacha kwa kuambiwa tu aangalie wenziwe au kutengenezewa mazingira ya ku-regret.. In case kama hufahamu Mkuu.. starehe ya utumiaji wa madawa ya kulevya na haswa cocaine na heroin unakuwa mwanzo tu wakati unapoanza kutumia.. Unakuwa unajisikia hali fulani ya ecstasy hivi.. Ila baadae sasa inabadilika na kuwa kama tiba.. Anapoyakosa madawa mtumiaji anakuwa na maumivu mwilini ambayo mwisho wa siku anashindwa kuyavumilia.. Hali hiyo inapelekea mpaka kuwa wagonjwa kabisa wenyewe wanaita alosto.. Wanapokuwa kwenye hali hiyo wanaweza kufanya lolote (hata kuliwa tigo) mradi wapate dawa ili wadevele..
Ushauri wangu kwa happiness win ni kutafuta rehab clinics ambazo wataweza kumsaidia mdogo wake..
pole sana
sie tuna mdogo wetu ameshindikana kabisa baada ya kuchelewa kugundua jutahidi kumpatia msaada mapema vinginevyo ni janga la familia
Polen sana,
Nijuavyo mimi bila yeye kuamua kuacha kutumia ni ngumu kumzuia asitumie
Oongeeni nae mpeni side effect ya hayo madawa then
akionekana anajutia ndo mumpeleke rehab
Asante kwa ushauri wako. Huyu Bwana mdogo amekuwa zoba kabisaaa, yaani tumeshakaa naye hana la maana analoongea zaidi ya kusinzia na kutoa udenda. Yaani unaweza kuongea naye mwenzio anainamaaa tu hadi analala, ila anadai yeye hajala madawa zaidi ya bangi. muonekano wake ni madawa tu yamemjaa akilini, na ameanza kuiba vitu na pesa nyumbani, kwa ndugu na majirani. Sijui nimpeleke hospitali gani?
Kabanga! pole tu! huna neno jingine la kunisaidia kuhusu hili? Asante
Asante sana. Ziko wapi hizo rehab?. Unaweza kujua gharama zake?
ndugu hili ni tatizo, samahani wacha nichukue nafasi yangu ya ualimu.
Mko mbali na mdogo wenu, hii ndio sababu kubwa sana, mwapasa kuwa nae karibu hata aikiwa huko shule ya bwalo.
tatizo lenu wazazi na walezi mnatuachia sana walimu kazi za malezi yote, kwa maana wewe ukishalipa ada eti umemaliza wajibu wako, lah, hapana kabisa kupitia kwa mwalimu waweza kuwa karibu sana na mdogo/mtoto wako, nasiku hizi mashule mengi yameweka siku za kuwatembelea watoto/wanafunzi tumia nafasi hiyo mzazi/mlezi, waweza jua mengi ya kijana wako kimaendeleo kiafya, kitaaluma n.k
Natumaini utakuwa umenielewa, vinginevyo uliza nitakusaidia...
Kuna hosp. Tanga inaitwa rutindi ni nzuri au rehab kwa hapa bongo sijui ipi nzuri.
ila hutaweza kumsaidia bila yeye kuwa tayari kuacha kutumia hayo madawa! Mkilazimisha treatment atatulia then atarudia tena! Ni vizur mkampa couselling had akubal kuacha ndio apate treatment.
kumpeleka shule mbali anaweza akasababisha matatizo mengne..kama ameshaanza udokoz ataibia wenzake akasake unga popote na hyo inaweza leta matatzo kwenu.
counselling ni muhimu, mnaweza kum encourage like kumwambia anaweza kuwa beta than condition aliyo nayo.
Mkuu hakuna mvuta unga aliekolea ambae aliacha kwa kuambiwa tu aangalie wenziwe au kutengenezewa mazingira ya ku-regret.. In case kama hufahamu Mkuu.. starehe ya utumiaji wa madawa ya kulevya na haswa cocaine na heroin unakuwa mwanzo tu wakati unapoanza kutumia.. Unakuwa unajisikia hali fulani ya ecstasy hivi.. Ila baadae sasa inabadilika na kuwa kama tiba.. Anapoyakosa madawa mtumiaji anakuwa na maumivu mwilini ambayo mwisho wa siku anashindwa kuyavumilia.. Hali hiyo inapelekea mpaka kuwa wagonjwa kabisa wenyewe wanaita alosto.. Wanapokuwa kwenye hali hiyo wanaweza kufanya lolote (hata kuliwa tigo) mradi wapate dawa ili wadevele..
Ushauri wangu kwa happiness win ni kutafuta rehab clinics ambazo wataweza kumsaidia mdogo wake..
Asante. umesema Lutindi iko Tanga? ni nitaitafuta. Nashukuru.