- Tunachokijua
- Samia Suluhu Hassan ni mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amekuwa akiendelea na kampeni zake katika mikoa mbalimbali nchini. Aidha leo Oktoba 01, 2025 ameendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro kunadi ilani ya chama hicho.
Madai
Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikionesha magari yaliyopata ajali kwa kugongana na kudaiwa kuwa ni msafara wa Rais Samia.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umejiridhisha kuwa video hiyo inapotosha uhalisia kwani haihusiani na msafara wowote wa Rais Samia bali tukio hilo lilitokea mwaka 2024 kwenye Msafara wa Paul Makonda alipokuwa Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM, ajali iliyotokea katika kijiji cha Sululu, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Februari 11, 2024 ikihusisha zaidi ya magari 10 yaliyokuwepo katika msafara huo.
Rejea hapa ambapo Millard Ayo alichapisha video ya tukio hilo na kueleza kuwa watu wasiopungua 7 walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara na kutokuwepo kwa kifo chochote.