AI_GURU
Member
- Nov 8, 2016
- 54
- 64
Video ya Magu NamibiaNimeona msafara wa Rais akiwa nchini Namibia. Hakuna walinzi wanaoning'inia hakuna watu wenye silaha za kivita.
Hakuna speed za ajabu kuwasha mataa na vingora vya hatari.
Nimeshindwa kuelewa tumeshindwa nini kuyatimiza haya nyumbani?
Ina maana hatuwaamini wanausalama wetu lakini wa Namibia tuna waamini?
Natumaini atakuwa amefungua macho kwa hii safari na atarudi na fikra mpya juu ya gharama za misafara yake.
Maswali ya kujiuliza ukiwa unajenga hoja:
1. Kama hofu ni ndani ya nchi inamaana Tanzania sio sehemu salama kuishi?
2. Kama anamaadui wengi itakuwaje kama asipochaguliwa 2020?
3. Nyerere na Magufuli ni yupi aliyekuwa strict kwa wabadhirifu na mafisadi?