Msafara wa makamu wa Rais waibiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa makamu wa Rais waibiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 19, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WATU wasiojulikana, majuzi usiku walivunja kioo cha gari ya matangazo iliyokuwepo katika msafara wa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein aliyekuwepo mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku tano na kuiba vifaa mbalimbali vilivyokuwemo katika gari hiyo.
  Taarifa za awali zinaonesha kwamba vifaa vilivyoibiwa ni kamera mbili ikiwemo ya picha za mgando na ile ya video pamoja na kumbukumbu zote za picha ambazo alikuwa amepiga toka mwanzo wa ziara hiyo ya Makamu wa Rais mkoani hapa.
  Kamera hizo zilizokuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 192 A zilikuwa zikitumiwa na Amour Nassor ambaye ni Mpiga Mpicha Mkuu wa Makamu wa Rais.
  vifaa hivyo vinadaiwa viliibwa majira ya saa 4 usiku muda mfupi baada ya gari hilo kuegeshwa katika hoteli ya Staff Inn mjini Iringa ambayo mwandishi wa makamu wa rais pamoja na waandishi wengine kutoka jijini Dar es Salaam walikuwa wamefikia.
   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  He he! Hata katika mji kama Iringa akili ya kawaida haikutumi kuacha vitu vyenye thamani kwenye gari.

  Bado tu Makamu wa Rais kuchomolewa simu mfukoni. Wananchi wana njaa!! Hawaogopi kuonjesha wakuu wa serikali joto ya jiwe!! (Ingawa sidhani kama mwizi alijua anamuibia nani)
   
Loading...