Msafara wa basi la Magereza leo umetia fora

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,964
20,813
Ilikuwa kama saa mbili na nusu hivi asubuhi ya leo, ambapo maeneo ya Kamata au tuseme Gold Star ulipita msafara wa mahabusu (kwa kuangalia gari la magereza) barabara ya Nyerere kuelekea City Centre. Msafara huo ulikuwa na pikipiki ya escort mbele kisha kufuatiwa na difenda za magereza kama kumi hivi, mbele ya basi zipo tano na nyuma zipo tano, na kwa haraka haraka kulikuwa na askari wanne ndani ya kila gari na kila mmoja alikuwa ameshika bunduki kwa pozi la kuelekeza mtutu tayari kwa kuachia risasi. Kwa maana hiyo msafara ulikuwa na karibu bunduki 40 kwa makadirio yangu.

Sijawahi kuona msafara wa kupeleka mahabusu mahakamani ukiwa na ulinzi mkali namna hiyo, kwa hiyo nimeshawishika kutafuta humu sababu ya ulinzi ule au pengine sababu za msafara ule. Anayejua zaidi anieleze kuna nini huko
 
Hao walikuwa ISIS jr. au ALS jr. !!
 
Hao askari wa Magereza waliopo kwenye huo msafara ni wale waitwao Kikosi Maalum cha Magereza " KM "

Hao ndio FFU wa Magereza, wako vizuri sana.
 
Waliokuwa kisutu watatupa majibu ata kuna kipindi moshi msafara Wa magereza ulikuwa unafunga njia kabisa mpaka farasi nadhani walikuwa wale majambazi walioiba NMB same na wale waliokamatwa arusha wakiwa Na silaha za kivita wakajifungia ndani jwtz ndio ilikuja kuwatoa
 
Mkuu hao ni wale magaidi ambao hua wanakesi kubwakubwa kama kupindua nchi au kama wale wafanya biashara haram kama meno ya tembo,wauza dawa za kulevya,, au wauwaji kama unavyosikiaga walioua ndugu zetu albino..n.k! Yaani hao escort huwa lazma iwe na vitendea kazi vya kutosha kwani hua ni watu hatari sana!!!na vilevile hata wao huwa na hasira sana maana kuna wengine labda wanasubiria ushahidi ukitimia labda wananyogwa hivyo hata wao tayari wanakuwa wanatafuta namna ya kujiondoa au kutoroka!!!ndo maana pale ulinzi hua ni full ngwamba!!!
 
Hawajiamini ndo maana kila kukicha ni vitisho tu, msafara wa kwenda dodoma nao ulikuwa ni kututisha tu! Ila wakae wakijua kwamba wanachokifanya sio sahihi na Mungu atatulipia sisi wanyonge!
 
Back
Top Bottom