Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by AbbyBonge, Mar 1, 2012.

 1. A

  AbbyBonge Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana tarehe 29 Februari 2012 nikiwa naendesha Rav4 (T601 BDD) majira ya saa 9;27 alasiri niliingiza gari yangu katika kituo cha daladala cha Msimbazi pale Kariakoo ili nimshushe mtu niliyekuwa nimeongozana naye. Baada ya kumshusha abiria wangu, nikapata wazo la kushusha vioo vya madirisha ili nipate upepo halisi kabla ya kuendelea na safari.

  Ghafla vijana wawili walifika dirishani kwangu na kujitambulisha kuwa wao ni Maafisa kutoka kampuni ya Udalali (TAMBAZA AUCTION MART) Iliyopewa Zabuni na Manispaa ya Ilala kukamata magari yaliyoegeshwa vibaya (Wrong parking) Kwa mshangao nikawajibu wale vijana mimi bado sijaegesha gari nimeshusha mtu na ninaendelea na safari, ndio maana bado nipo katika uskani wa gari yangu na sijazima injini.


  Kwa masikitiko makubwa hakuna aliye nisikia wala kunielewa, na kwa pamoja wakafungua milango ya gari na kuingia ndani ya gari, kisha wakaanza kuniamrisha niendeshe gari kuelekea wanakotaka. Kwanza wakaniambia niingie mtaa wa Swahili na kabla ya kufika makutano ya Swahili na Mafia wakaniambia simama utuambie tukusaidie vipi. Nikawajibu sina pesa kama mnataka mniache tu maana sioni kosa langu. Wakaniambia endesha twende Msimbazi Polisi.


  Niliposikia Polisi nikaona safi maana nitakutana na watu wanaojua wajibu wao tofauti na niliofuatana nao. Cha ajabu tulipofika msimbazi wakasema usiingize gari ndani paki hapo ( yaani pale nje) maramoja wakashuka na kuifunga ile gari na lile chuma lao sasa kama vili Gari imekutwa imeegesha hapo. Angaongezeka Kijana mwingine ambaye walimtambulisha kwangu kwa jina la Abdul na ni bosi wao.


  Abdull naye nilipotaka kuanza kumuelezea kuhusu huo uvamizi wa vijana wake hakutaka kunielewa kabisa na akaniandikie karatasi kwa ajili ya kwenda kulipia Tsh 100000/=. Nikawauliza kama kuna bosi wao mwingine nizungumze naye, wakaniambia subiri kidogo anakuja. Baada ya dakika chache akaingia dada mmoja nahisi nilisikia wakimwita IRENE (Sina uhakika na jina hili) Nikamuomba niongee naye pembeni akasogea na kunambia kwakuwa nimeisha andikiwa hawezi tena kufanya lolote lazima nikalipe. Papo hapo akaniuliza aite Break down livute gari yangu ama nitaendesha mwenyewe. Nikamjibu nitaendesha mwenyewe. Nikaambiwa haya endesha gari twende Anatogro kwanza na labda naweza kukusaidia tukiwa huko. Hapo sasa vijana wane wakaingia katika gari yangu badala ya wale wawili.


  Vijana hao wanne walipoingia tu garini, walianza kulipekua gari langu, mmoja akaona Kisu kikubwa pale pembeni akakichukua na kukipeleka katika gari la bosi wake, Yule aliyekaa mbele akawa bize na redio akibadili stations, wale waliokaa nyuma nao kadhalika walikuwa wakipekuapekua huku tukielekea Anatogro. Kumbuka hii sasa ilikuwa inakaribia saa kumi na moja kasoro kidogo na walikuwa wanatakiwa kurudi Anatogro so waliitumia gari yangu kama STAFF VAN.

  Tulipofika Anatogro wakalifunga tena gari langu na mara moja wakaniambia wamepigiwa simu Kariakoo kuna mtu anakata nyororo lao hivyo niwasubiri. Wakaondoka na kuri tena majira ya saa moja na robo usiku. Hapo sasa wakaniambia nichague kulipa elfu hamsini badala ya laki moja, nilipo waambia sina pesa hiyo, Yule dada akanambia nichangue waite break down au niendeshe mwenyewe mpaka Yard yao iliyopo Mamndela road. Mikachagua kuendesha, akanipa kijana wake mmoja anipeleke huko, Tulipofika Buguruni nikaingiza gari polisi nikataka kuomba msaada, kabla sijashuka Yule kijana akanambia usiende Polisi huyo mkuu wa kituo hapo ni swahiba yetu mkubwa na tunakula naye huu sisi ndio mchezo wetu siku tukikosa magari yenye makosa, Nakuona ni mpore na sio mtata ndio maana nimeona nikwambie ukweli ili usipate usumbufu zaidi. Alisema Yule kijana.

  Nilimuelewa Yule kijana na nikamwambia basi twende Sinza nikakupe hiyo elfu hamsini ili msiingize gari Yard. Akakubali na tukaelekea Sinza nikaenda kumpatia hiyo pesa na tukaachana , yapata saa tatu usiku.

  Choka mbaya na hasira, nikaanza safari ya kuelekea nyumbani Temeke. Nafika nyumbani nakumbuka simu yangu iliisha chaji mchana na niliiweka katika mfuko wa koti nililolitundika nyumba ya kiti cha dereva siioni. Nazidi kupata hasira kuwa wale vijana wameniibia simu. Nikarudi garini kuangalia vizuri ili kujua nini kingine hakipo, nikagundua na ile flash disk niliyoiweka pale kati ya kiti cha dereva na abiria, kwenye kile kishimo cha duara (wanaoendesha Rav4 wanapapata vyema) nayo sikuiona, vijana wamekula.

  Asubuhi ya tarehe 01.03.2012 nikawahi pale Anatogro kuulizia ofisi za Tambaza Auction Mart, naambiwa hawana ofisi pale, wana Muhasibu tu. Nikamfuata Muhasibu kumuuliza ofisi yao akasema kwa sasa kampuni yao haina ofisi ila nimpigie Mkurugenzi wao anaitwa Abdallah akanipatia nambari ya simu ambayo niliipiga bila kupokelewa hadi kunakuchwa. Lengo langu awatangazie Staff wake wanilrejeshee japo ile flash maana ina mambo muhimu kuliko ninavyoweza kuelezea.


  Nimemalizia siku yangu kwa kupita Msimbazi Polisi kufungua jalada la wizi dhidi ya Kampuni hii.


  Jee,

  a)
  Ni wakati gani mtu anakuwa ameegesha vibaya,

  b) Ni wapi gari lilipaswa kufungwa ikiwa liliegeshwa vibaya? Ni pale nilipokutwa au kule nilikopelekwa?
  c) Mipaka ya Maofisa wakamataji inaishia wapi nje ya gari au mpaka ndani pamoja na kupekua?
  d) Naanzia wapi kudai haya yote niliyofanyiwa?
  e) Nk.
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Hiyo 50,000 uliyompa alikupa risti?tuanzie hapo
   
 3. A

  AbbyBonge Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndiyo risiti ninayo, niliifuatilia siku iliyofuata.
   
Loading...