Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mutta, Jan 19, 2012.

 1. Mutta

  Mutta Senior Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rafiki yangu amekuja kuniomba ushauri mgumu,nikaamua niwashirikishe.Yeye ameoa ana miaka 6 kwenye ndoa ya kanisani.Hawana mtoto mpaka leo.Wameenda kupima yeye ni mzima ila mkewe ana matatizo{sijui kama ni ya kudumu au la}.Anataka kutoka nje ya ndoa ili apate mto to maana amejenga nyumba.Wote wana kazi ila mwanaume anachekwa kuwa labda jogoo hawiki.Je nimsaidieje au Ungekuwa wewe una tatizo kama hilo ungefanyaje?
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wakae chini wote watafute ufumbuzi, Kama wote nia yao moja mwwnyezimungu atawajaalia,kwenda njee ya ndoa sio jawabu zuri endapo mkewe akijua na hakuomba kua hivyo sass asimsugue roho mwenzake...
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanza miaka sita, sio mingi sana kwa hesabu za sikuhizi. Labda tatizo umri ukiwa umesogea kujaribu kunaweza kuwabana kidogo. Pili, hilo ni swala gumu sana, tena kujadili kwa kusikia upande mmoja tu! Unahakika mkewe anahitaji mtoto pia? Tatu, mwenzio anapaswa kukuambia wazi nini maana ya mtoto. Ni yule wa damu yake tu ama yoyote watakae lea?
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  1..kujenga nyumba si kiegezo kwamba anapaswa kuwa na mtoto/watoto

  2.... ndoa siku zote haihusiani na watoto yale ni matunda ya ndoa na ndio maana kanisani huwa wanasema ..je mko tayari kuwalea na kuwatunza watoto MTAKAOWAPATA?....kumbe mnaweza kuwakosa pia

  3...kutoka nje ya ndoa ni kuongeza matatizo

  4..akae chini na mkewe waongee na kama mke akikubali hoja ya mzee sawa ....

  5....waende vituo vya kulelea watoto yatima waadopt mtoto/watoto
   
 5. Mutta

  Mutta Senior Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaoneka umri wa mwanaume umesogea kwenye 40 hivi na mke 30 .Sasa yeye anaona umri umeenda kila akijaribu anabaki ola. Je mke atakubali mwamme atoke nje.Je mali walizonazo {nyumba,gari} atarithi nani
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Mwanamke akishaelewa kwamba ana tatizo na nila kudumu, anaweza kukubali.... hadi huyo mama ajue/akubali hilo,mumewe hastahili kwenda kutafuta mtoto nje ya ndoa....watu wanakaa miaka mingi sana....maombi maombi!!
   
 7. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,370
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Umri kitu gani bwanaaa. Aachane na mambo hayo. Akae na mke wake kwenda nje sio kigezo cha kupata mtoto.
  Kama wamefunga ndoa kanisani waliapa wakasema watavumiliana kwenye shida na raha.
  Kumbuka Ibrahim alipata mtoto akiwa na umri mkubwa sana.

  Mwambie amgoje Bwana natafanya yeye aache njia za mkato, atapata matatizo badala ya kusolve
   
Loading...