msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada

Discussion in 'JF Doctor' started by Uzuri, Apr 28, 2011.

 1. U

  Uzuri Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nnajamaa yangu anatatizo la kushindwa kufanyakazi kwa figo.hali inayompelekea kuishiwa damu mara kwa mara ,je kwanini damu huisha mara kwa mara na je suluhisho ni nini ukiondoa kubadilisha figo?. Kumbuka mafigo yote ma2 yamefail..
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Pole Uzuri...ukifuatilia thread yenye kichwa kinachosema 'ERYTHROPOETIN 4000IU SC Dawa ya FIGO' utakuta comment zinazojibu swali lako.

  Mafigo kwa kawaida huwa yanatoa kichocheo kinachoitwa 'Erythropoietin', hiki kichocheo hustimulate bone marrow kuzalisha chembe chembe nyekundu za damu (red blood cells). Mafigo yanaposhindwa kufanya kazi (mafigo yote mawili, maana figo moja inatosha kufanya kazi za figo mbili katika mwili wa binadamu) basi hiki kichocheo hakitolewi, na hivyo bone marrow haizalishi red blood cells inavyotakiwa. Hii inasababisha mgonjwa kupungukiwa na damu mara kwa mara na kulazimika kuongezewa kwani hata akimeza dawa za kuongeza damu hazitamsaidia.

  Kwa hiyo kama vipimo vikithibitisha bone marrow inafanya kazi (bone marrow aspiration/biopsy), basi mgonjwa atahitaji apate sindano za Erythropoietin ili bone marrow ziendelee kuzalisha red blood cells na mgonjwa asipate upungufu wa damu.
   
Loading...