Msaada - ZANA ZA KILIMO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada - ZANA ZA KILIMO

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mgombezi, Feb 16, 2011.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  Ningependa kufahamu upatikanaji wa Zana mbalimbali za kilimo na usindikaji wa mazoa; matumizi, bei yake, picha (kama inapatikana) na mahali inapopatikana (zile ambazo zinapatikana hapa nchini).

  Zaidi napenda kufahamu ninapoweza kupata mashine ya e kupukusa mahindi.

  Asante kwa michango.
   
 2. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa yeyote anayefahamu mahali ninapoweza kupata mashine ya kupukusa mahindi ya kutumia mkono.
   
 3. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante sana mgombezi kwa swali. Mimi naomba mpira huu niwatupie vijana wetu hapo CoET, DIT, St. Joseph luguruni, etc.... Hii ni opportunity ambayo emerging mechanical engineers wanaweza kuitumia kujipatia kipato mara wamalizapo shule.
  Sasa naomba mmoja achukue project title hii na afanyie kazi "design and construction of a tangential maize grain thresher for a Tanzanian farmer". Wakati unafanya engineering considerations, hakikisha gharama ya mashine hii inaweza kununuliwa na mkulima wa kawaida lakini itakuwa na uwezo mkubwa wa "kupukusa" mahindi kwa kasi kuliko mikono BILA KUVUNJA GRAINS. Utapata "A" yako kwa sababu unafanya kitu kinachoendana na hali halisi na pia kinasupport gvt priorities juu ya "kilimo kwanza" na pia utajipa mshiko baada ya kumaliza chuo maana utakuwa unafyatua na kutuuzia mashine hizi bila kuhitaji kujikaanga na interview na kuishia kulipwa laki 2.
   
 4. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mkuu pale morogoro kuna jamaa wanaitwa INTERMECH, wanapatikana Kihonda Industrial Area wanamachine za aina mbalimbali including hiyo unayoitaka
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ... wazo zuri sana hili....kama changamoto ... je kuna programs zitakazoweza ku support kama hii project itakuwa feasible...? kwani fresh from college vijana hawana resources za ku implement successful project ideas....?...je wahadhiri hawataiweka project hii kapuni tuu as an academic publication...? pia kuna protection au patent rights zipi as an emerging mechanical engineer atahakikishiwa ili aweze kubenefit trade mark yake ... nilishauri tuwe na program za empowerment ya innovations au creativity ya vijana watakaoonyesha ujasiri wa uanzishaji wa technologjia rahisi kama huu ulio upendekeza

  tupo pamoja mkuu
   
 6. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante THE PLANNER; kwa taarifa hii, nimewatafuta na kuwasiliana nao na wamenieleza mashine ya kutumia diesel inagharimu Tsh 3,500,000/= na ile ya kutumia mkono ni Tsh. 650,000/=. Je hakuna wengine unaowafahau nikaweza ku-compare price, hata hivyo bado tuna safari ndefu katika kujikwamua.
   
 7. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu MUTENSA; wazo lako ni zuri sana, kwamba katika wakati huu ambapo serikali inajaribu kutoa kipaumbele kwa kilimo basi vyou vya ufundi vingeelekeza jitihada za kugundua zana za kilimo na usindikaji ambazo zitarahisisha uzalishaji.
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  tunarudi kule kule.. serikali huwa inaimba kuhusu empwerment watu watengeneze vikundi na waombe mikopo..wakitimiza masharti chenga zinaanza... kuna tatizo kubwa katika kufanikisha sera hii ya uwezeshaji..!!Vijana waichue kama changamoto ya kitafiti na ikifanikiwa watu watawekeza katika ulishaji..!!
   
 9. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wadau; hitaji langu ni zile zana ambazo kwa sasa zinapatikana; hivyo napenda kufahamu - duka au mahali ambapo naweza kupata zana za kilimo na usindikaji wa nafaka mbalimbali; lakini uhitaji wangu mkumbwa ni mashine ya kupukusa mahindi.
   
 10. bab-D

  bab-D JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2015
  Joined: May 2, 2015
  Messages: 1,130
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pesa zinakamatwa ktk kapeni kwaajiri ya kuhonga washinde badala ya kuwekeza ktk ubunifu kama huu, tabu sana tz
   
 11. kiogwe

  kiogwe JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2015
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 3,220
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Bab-D na wanajukwaa wengine naweza kupata wapi hii dawa ya magugu inaitwa Round Up kwa bei za jumla.kariakoo sokoni juu naona wananiuzia kwa bei za rejareja naomba kuelekezwa duka
   
Loading...