Msaada wetu uko wapi Watanzania?

Philibert Buyobe

New Member
Joined
Aug 26, 2019
Messages
4
Points
45

Philibert Buyobe

New Member
Joined Aug 26, 2019
4 45
Wapendwa wana JF nimeleta haya bayana mbele yenu,
Kwanza nipende kupongeza Sana kwa yale yanayoendelea hapa Nchini na zaidi chini ya jemedali kiongozi wetu JP.Magufuli, kwani mambo mengi maovu sasa ameyadhibi kwa asilimia sitahiki, maovu Kama ufisadi,rushwa na kuleta nidhamu kwa wafanya kazi wa umma katika ofisi mbalimbali.
Watanzania wenzangu wengi wetu tunajikita kwa kuwasaidia Wale ombaomba walioko mitaani na wengine wamekaa katika kando za barabara, kwa ujumla ni jambo jema. Sasa mimi nakuja kwa hawa ambao unakuta kijana na nguvu zake anamtoa mtoto au mtu yeyote mlemavu na kumbeba kwenye kibaiskeli chake na kisha kuanza kumpitisha huku na huku ili watu wamwonee huruma na kumchangia chochote kile.Watanzania katika hilo nawaambia tunakosea Sana kuwasaidia watu Kama hawa, kwa nini tusiwakamate hawa watu na ikiwezekana watafutiwe namna ya kufanya kazi ili wapate kipato cha kuwasaidia hao walemavu? Kuna kazi nyingi tu wanazoweza fanya mojawapo serikali inaweza wakamata na kuwapa kazi kwenye mashamba na kuhakikisha wanafanya kazi, itafikia wakati hawataona tena kuwa wanaumia na badala yake watashukuru kwani watakuwa wamefumbuliwa akili zao.hilo ni moja ya pendekezo langu mengine unaweza kuongeza ili tuwasaidie ndugu zetu hawa, Inaumiza Sana ukigikilia kwa kina juu ya hili halafu unakuta na sisi tunafurahia tu kuwapa hela, Serikali ikiwezekana itafute namna ya kuwasaidia na hii itapunguza ongezeko la Ombaomba katika miji yetu
Kwa Leo nipo hapo tu, Mungu awabariki
 

Forum statistics

Threads 1,378,926
Members 525,244
Posts 33,728,436
Top