msaada wenu wa haraka na ushauri unahitajika sana

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,223
kwanza natanguliza heshima kwenu wakuu.
wakuu naomba msaada wenu napata tabu sana .shida yangu ni kuwa ninaredio sasa kunasehem huku nimehamia nahisi umeme ni kidogo sababu ikifika usiku tu redio haiwaki kabisaa na ikizima pale kwenye screen yake inaandika high voltage hii hutokea kama ulikuwa umaiacha ON na kama ulikuwa umeizima na kama utaiwasha haiwaki kabisa na kama itawaka basi inazima hapo hapo.
sasa kuna kauchunguzi na majaribio nimefanya kule nyuma ya redio unapoingia waya wa power kuna switch ya power ya kuselect kuna 120 V
220 V
240 V
nilijaribu kuihamisha na kuiweka kwenye 220 V bado ikagoma nikaiweka kwenye 120 V ikawaka bali nikaizima hapo hapo huku nikiwa na wazo kichwani kama nitaiweka hapo kwenye 120 V naikatokea gafla umeme ukarejea kama kawaida nini kitatokea? je redio si inaweza kuungua?.
mwisho na shida yangu ni kuwa nitawezaje au nifanye nini ili niweze kutumia redio hii katika condition hiii nini kinahitajika kifanyike ili niweze kuendelea kuitumia kama kawaida? naomba msaada wenu wakuu?
 
Kwanza kabisa hizo voltage zimewekwa mahususi ili bidhaa hiyo iweze kuuzika na kutumika katika nchi mbali mbali kwa sababu kuna nchi nyingine kama marekani wao voltage yao mwisho ni 120 hivyo kama bidhaa hiyo isingewekewa uwezo wa kuswitch to 120v then bila shaka hiyo redio isingiweka endapo ingetumika katika nchi zenye maximum voltage ya 120 kama marekani.

Kwa huku Bongo maximum voltage yetu ni 220 hivyo kitendo cha kuset voltage ya hiyo redio kwenye 120 kunaweza kusababisha kuunguza redio yako endapo umeme utarejea katika hali ya kawaida hivyo nakushauri urejeshe redio yako kwenye 220v. Kama hilo tatizo la umeme mdogo linakukera na linakufanya ushindwe kufurahia kutumia redio yako basi nakushauri ununue UPS ambayo yenyewe ndani yake huwa ina backup battery ambayo itakusaidia kuifanya redio iendelee kufanya kazi kwa muda flani endapo umeme utakuwa mdogo au utakatika kabisa. UPS ndogo kabisa nadhani unaweza kuipata kwa Tshs.80,000 tu.
 
Back
Top Bottom