mi nakupa mchango wa mawazo.
unaweza tafuta rafiki zako ambao unataka wawe wasimamizi (wadhamini) wako wa ndoa.....
nenda nao unakopanga kufunga ndoa (msikitini, kanisani, kwa DC, nyumbani..........), huko kote wanaulizia wadhamini wa ndoa tu.....
mkimaliza hapo mnatawanyika au mnaenda kupata lunch/diner...... umemaliza kazi
wala huhitaji kuumiza kichwa kwa hili mdogo wangu
Kiukweli Madada Mnatuumiza sana
Nilipe mahali (unakuta Mbaba unataja tu Ng'ome kumi na mbuzi sita na mkaja sijui (2000,000) totall
Nimekutaftia kazi, unapata mshahara bado tu unataka kuniumiza kunifanyisha harusi ya expensive
eti anatimiza matakwa ya mke mtarajiwa!
hajui huwa hayaishi hayo.....
akianza leo kudai harusi kubwa wakati anajua huna uwezo ukamtekelezea kwa kuitisha harambee JF na FB kesho atakuja na jingine
eti anasema ni special day.... hairudiagi....Umenikumbusha mdada alikuwa ndo kwanza kamaliza udsm afu jobless na anaolewa. Yule kaka nahisi koromeo lilimkauka maskini! Manake pete iliyakiwa ya yakub's na viatu vya mariedo. Nilimuangalia sikummaliza!
huko unapoishi lazima kuna marafiki,ndugu na majirani waliokuzunguka
ni kweli ndoa ni tukio kubwa sana,andaa kadi za michango,gawa kwa marafiki na ndugu,na wale ambao ww ushawachangia,nina imani ukiongeza na kidogo ulichonacho utafanikiwa kile unachataka kiwe,kila la kheri!
Ushauri wako ni mzuri sana Passion Lady, nitauzingatia, lakini hata wewe unanafasi katika hili
Kwasababu Watanzania wote ni ndugu,