Baada ya kumsilimish ulitakiwa
Usimuache baada ya hapo, ungempa vitabu vya Dini, unge mfundisha Dini vizuri, ikiwa wewe hujui ungemtafutia Mwalimu japo umlipe aweze kumfundisha Uislam.
Makosa makubwa yanafanywa sana na Waislam, ni kuwa baada ya kumsilimisha mtu humwacha akaenda zake na hawamfuatilizii wala hawamsaidii kumfundisha Dini wala kujua kama anaswali, anafunga n.k. Jaribu kumsaidia kwa hali na mali kadiri uwezavyo .
Pia makosa makubwa yanatokea kwa kuwa wale wanaowasilimisha watu au kusababisha wasilimu, wao wenyewe hawatekelezi mafundisho ya Dini, hawaswali, hawana tabia njema za Kiislam na hata hawaijui Dini yao wenyewe. Jambo hilo huja kuwachanganya sana wanaosilimu, kwani wanakuta Uislamu unasema vingine na Waislamu wanafanya vingine!
Na ikiwa ni mtu ambaye hufuati mafunzo ya dini yako kamili, basi hukuchelewa sana, nakusihi, uanze kutekeleza na kujifunza kwa kusoma au kuhudhuria madarsa na mihadhara ya Dini n.k. kwani usipofanya hivyo ujue kuwa mkeo huyo uliyemsilimisha amesilimu jina tu lakini kivitendo hatopata mafunzo na mifano kutoka kwako atabaki kama alivyokuwa katika ukristo wake kwani anakutegemea sana wewe khaswa kwa kupata mafunzo ya dini .