Msaada wenu tafadhari juu ya afya ya mwanangu

Habari ndugu zangu wiki kama moja iliyopita mwanangu alilazwa na akachomwa sindano nyingi sana mikononi ni mtoto wa miezi 11.

Sindano zile zilimpelekea kuvimba mkono kwa juu nilivyowauliza hospital wakanijibu hali hiyo itaisha nimesubiri kwa muda wa siku nne sioni dalili za hali hiyo kuisha nikamua kwenda private hospital kupata ushauri.

Nikaambiwa kuwa inabidi apasuliwe mkono maana wanadai kuwa ndani pametengeneza kama jipu.
Nikawajibu acha nirudi kesho.

Kabla sijachukua maamuzi nikaona nitafute Dkt mwingine anipe ushauri pia yeye akaniambia kuwa mtoto kama huyo mishipa yake ni midogo sana kwahiyo kupasuliwa kunaweza kusababisha madhara zaidi akanipa dawa kuwa itamsaidia.

Sasa hapa nimebaki njia panda nimeona nije kwenu hapa maana naamini hapa kuna watu wengi wenye ujuzi na elimu tofauti asanteni.

View attachment 2944366
Mtoto amepona?
 
Niliwahi mziba nesi vibao mana si kwa jinsi alivonijibu tena akiwa na gomba anachanja na anapaswa muhudumia mtoto sindano
 
Back
Top Bottom