Kuna watu wengi wanapotoshana sana kuhusu hizi Android Smartphones, yaani kukitokea tatizo dogo mnashauriana kureset simu.
Ishu ni kwamba unapofungua email ile username yako hutoitumia tena utakapotaka kufungua, na hata mtu mwingine akitaka kuitumia hiyo username haitaweza kutumika kwa kuwa inexist kwenye google servers na database. Kwa hiyo kama utapenda kutumia username hiyo itabidi uongeze baadhi ya herufi au namba kufanya hiyo username iwe unique.
Kwa mfano, mtu akajisajili email kwa kutumia username ya "justjose@gmail.com" username hii haitotumika tena. kwa hiyo mtu nwingine atakapotaka kutumia username hii wakati wa kujiandikisha email hii, atalazimika kutumia username nyingine au akaongezea tarakimu katika username yake ili iwe ya kipekee.