Msaada wenu ili niweze timiza ndoto zangu

monotheist

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
720
943
HABARI ZENU WAKUU,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kigogo jijini Dar es salaam nimemaliza kidato cha sita mwaka 2016 tahasusi ya HKL on lipata division 3, points 14 yaani D, E, E na F hivyo sikuwa na sifa ya kusoma chuo kikuu

Lakini sikukata tanaa baada ya matokeo nikaamua kutafuta kazi ili niweze pesa ya kurudia baazi ya masomo hivyo nikafanikiwa kupata kazi ya usafi ktk kampuni Fulani hapa jijini

kutokana na hali ngumu ktk familia kaka zangu walishindwa kunitimizia mahitaji yangu ya shule hivyo nikaamua kupambana mwenyewe kama mtoto wa kiume, mshahara wangu wa kwanza nililipia mtihani pamoja na kituo cha kufanyia mtihani.

Nashukuru mungu matokeo yangu yalikuwa mazuri nami nikawa mmoja miongoni mwa manafunzi wenye sifa ya kusoma chuo kikuu na ndipo nilipoanza udahili huku nikiwa natafuta wazamini wa kunisaidia ktk gharama za ada ya chuo.

Huku nikiwa naendelea kufanya kazi ya usafi nilipatachangamoto nyingi sana japokuwa si Mara ya kwanza kufanya kazi ya usafi nilishawahi kufanya baada ya kumaliza kidato cha NNE wakati nasubiria matokeo ya kidato cha NNE

Baazi ya wafanyakazi wa kampuni niliyokuwa nafanya kazi walikuwa wananidharau na kunishusha thamani pia baazi ya watu niluokuwa naishi nao mtaani waliponiona nawajibikavktk kazi yangu walinicheka na kunza kunisimulia mtaani ilifika wakati nafanya kazi huku nalia kutokana na maneno ya watu lakini yote nilivumilia.

Kiasi Fulani nilikua nafanya kazi katika mzingira magumu nilikua nasafisha vyoo nakama unavyojua wengine gawana ustaraabu wanapokua chooni, nilikua nasafisha ofisi ,mandhali ya nje na kuosha magari ya tajiri zaidi ya matatu kwa siku katika jua Kali kama unavyojua jua la Dar linavyowaka lakini yote hayo nilivumilia nilijua nini ninachokitaka.

Hatimaye nikakutana na tajiri wa kampuni ambaye ndiye mmiliki ili awezekunisaidia gharama za ada ya chuo nashukuru alikubali japokuwa hakunambia kiasi atakachonipa.

Ndoti yangu ni kusoma sheria na kujiajiri ktk biashara ndogondogo kisha biashara Kubwa pia lengo langu ni kusoma huku nikiwa nafanya biashara. Hatimaye nikaamua kuacha kazi ili nifanye maandalizi ya kwenda chuo kwa kua muda wa kazi ulikua ubanibana.

Bahati mbaya pale ofisini ulitokea wizi wa Mali yenye thamani ya Tsh milioni 32 ilipelekea yule tajiri kuwa na mawazo mengi sana zidi ya wizi uliotokea Hatimaye akanipatia Laki 5 kama sehemu ya mchango wake.

Huku nyumbani napi mambo magumu hakuna wa kuniongezea nami Nina laki 5 mkononi nikapata wazo la kuanzisha ufugaji wa kuku ili niweze kuizalisha ile laki 5. kwa kua mzee wetu amejenga hapa jijini ndipo nilipoanza ujenzi wa banda dogo la kuku.

Hatimaye pesa imeisha na banda bado hakijakamilika ndipo nilipochukua uwamuzi wa kuuza simu yangu ya mkononi humuhumu Jamiiforums na kupata Tsh 180,000 na kupangisha chumba changu kwa Tsh 180,000 kwa miezi 6 jumla nikapata Tsh 360,000 ndipo nilipofanikiwa kumaliza banda.

Pesa kidogo iliyobaki nikanunua vifaranga vya kuroila 47, vifaa vya chakula pamoja na chakula cha kuku lakini nilipata changakoto Kubwa ya magonjwa na vifo vya kuku kwa kukosa pesa ya kununua madawa ya kuku Hatimaye nimebakiwa na kuku 4 kati ya kuku 47

Nguguzangu nahitaji msaada wenu wa hali na Mali kutimiza ndoto zangu. Nahitaji kazi yoyote hasa kazi ya kuuza duka ili niweze kujifunza changamoto za biashara kwani ndiyo ndoto yangu. Kwa sawa sina wazo la kurudi shule nataka nitimize ndoto yangu ili nisaidie familia kwa sasa kula yetu ya kuungaunga tu cha kushukuru ni kwamba mzee wetu amejenga mjini tutazunguka lkn pakulala tunapo.

Msaada wenu wakuu nhitaji kazi nimeshahangaika sana lkn sikufanikiwa.

Kwa yeyote atakayeguswa na kutaka kunisaidia tafadhali asini-PM sababu sina simu yenye internet.

Kwa mawasiliano 0692402211


NATANGULIZA SHUKRANI
 
Pole ni changamoto tu za maisha,

Umeona ID yangu hiyo picha ukikubali kufuatana nami nikupeleke nyuma ya jengo la hoteli ya kilimanjaro, am sure hutateseka utakuwa mtu wa kuendesha magari ya kifahari. welcome to the real world.
 
Pole ni changamoto tu za maisha,

Umeona ID yangu hiyo picha ukikubali kufuatana nami nikupeleke nyuma ya jengo la hoteli ya kilimanjaro, am sure hutateseka utakuwa mtu wa kuendesha magari ya kifahari. welcome to the real world.
Ahsante mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom