Msaada wenu nataka kumkamatisha polis rushwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wenu nataka kumkamatisha polis rushwa.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by LEGE, Dec 27, 2011.

 1. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Msaada wenu wakuu mim nikijana najishughulisha na kazi ya ufundi umeme wa magari.Wiki iliyopita nilikuwa na rafiki yangu tumebeba engine control tulikuwa tumetokanazo kariakoo kwa mafundi wenzetu.Tulikuwa tumetoka kuzichukua tukajalibu kuwashia gari tuliyokuwa tunaitengeneza na kama tutafanikiwa kuiwasha tutarudi tena kule tulikozichukua ili tuongee biashara.
  Kwa bahati mbaya au nzuri kabla hatujafika nazo gereji tukakutana na polisi wakatukamata na kutupeleka post tulipofika post wakatutaka tutoe hela laki 2 ili watuachie pamoja na mali zetu.
  Bahati mbaya fedha hizo tulikuwa hatuna tukampigia sim fundi mwenzetu akaja akatoa 30 elfu tukaachiwa na mali zetu tukaziacha.Kwa masharti yafuatayo kama tutaenda na risit ya kumiliki mali hizo tutapewa bure bila malipo yoyote.

  Kama hatutakuwa na risiti basi tuende na raki 2 ilitupewe mali zetu.

  Ugumu ni kwamba sie risit hatuna kwani engine control nyingine tulienda kuazima kwenye gari ya mtu na sasa imekuwa tabu wenye mali wanadai.Na uwezo wakuzilipa sie hatuna.

  Hivyo tunataka tukachukue hela za pcb na tuwapelekee hizo laki 2 ilitupate mali zetu.
  Swali je kama tutawapa hera hizo za rushwa tutapata mali zetu ??
  Naomba msaada wenu wakuu lasivyo ntafungwa mim.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mkuu kua makini hata hao pcb hawaaminiki cha msingi kama ni kweli hayo maelezo yako mtafute mwanasheria yeyote mlipe hata buku30 kwa kukusindikiza na pcb waambie kabisa huyu ni mwanasheria wangu ili wasijekushirikiana na askari wakakunyang'anya mali wote hao pcb na police ni watoto wa baba m1 mama m1 so hawawezi geukana
   
 3. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Fanya kama alivyosema King Kong mzee wa Regae. Huyo mwanasheria anaweza pia kuwasaidia kuzitoa hizo mali zenu kwa kuwa si kosa kupatikana na spea ya gari ikiwa tu unaweza kuthibitisha uhalali wake. Kama unakwenda sehemu kusafisha pump polisi wakikukuta na pump watadai risiti utaitoa wapi?

  Lazima kuna udhaifu mmeuonesha ktk kujibu maswali yao na ndio maana wanatake advantage kuwakandamiza. Hamna kosa waungwana, spea ya mwili tu ndio kosa kupatikana nayo.
   
 4. m

  mhondo JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Sidhani kama ni kweli polisi na pcb ni baba 1 mama 1 isipokuwa ni hofu ya kuzusha ugomvi ambao hatimaye inaweza kusababisha matumizi ya silaha za moto. Inategemea hao polisi wanataka wapewe hizo hela mahali gani? Kama ni kituoni kwao ni ngumu kwenda kuwakamata bila kushirikisha polisi wenzao na hasa waliowazidi cheo hao wahusika.
   
Loading...