Msaada wenu jamani, sikio linanisumbua

Msaada wenu jamani, sikio linanisumbua

Cappadonna

New Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
3
Reaction score
0
Ndugu zangu habari za Saa hizi, naomba msaada wenu, sikio langu la kushoto lilianza kuwasha sana wiki nzima, sikulitilia mkazo kulishughulikia, sasa hivi hali imekuwa mbaya, naona linatoa maji fulani hivi mepesi lakini8 yana harufu kali sana mpaka najiskia vbaya kukaa pamoja na watu.

Je, kuna dawa yoyote naweza kutumia?

Msaada tafadhali
 
Ndugu zangu habari za Saa hizi, naomba msaada wenu, sikio langu la kushoto lilianza kuwasha sana wiki nzima, sikulitilia mkazo kulishughulikia, sasa hv hali imekuwa mbaya, naona linatoa maji fulani hv mepesi lakin yana harufu kali sana mpaka najskia vbaya kukaa pamoja na watu.

Je kuna dawa yoyote naweza kutumia?

Msaada pliz
Pole kwa kuumwa,
Kwa sikio ambalo limeanza kutoa majimaji, ni dalili pia ya kuwa kunaweza kuwa na usaha.

Si vyema kutumia dawa ya kudondoshea/matone. Kwani dawa za aina hii huenda kutuama juu ya usaha na kuwa chakula sehemu ya kuzaliana bacteria. Hivyo, kufanya zisiwe na athari chanya.

Njia nzuri ni kupata dawa za kunywa ili zikafanye kazi kupitia mfumo wa damu.
Dawa za familia ya Ampicillin/Amoxylline/Amoxyclam ni moja ya dawa zinazotumika pamoja na dawa ya kutuliza maumivu.

Ni vyema kufika hospitali ili kujua hali ya sikio lako na utumie dawa kwa siku kiasi gani ili kumaliza tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom