Enny
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 962
- 130
Wana JF naomba mnisaidie katika hili . Nina lori linafanya biashara za kusafirisha mizigo kwenda mikoani. Lakini toka limeanza kufanya biashara faida yake haionekani. Kwenda na kurudi mapato ni milion mbili, matumizi ni diesel huwa kwenye mil. 1.5, udalali na upakiaji ni laki moja. mizani ni kama elfu arobaini na allowance ya dereva ni laki hamsini. najikuta kama nabakiwa na laki mbili, na hapo lazima nitoe hela ya lubricants, matengenezo madogomadogo. Sasa nikipiga mahesabu naona hamna faida kwani gari likitakiwa matengenezo makubwa najikuta naenda kuchukua hela ya mshahara kutengeneza, hapo bado kodi mbalimbali za TRA, SUMATRA, n.k.
Naomba mtu mwenye uwezo wa kuendesha hii biashara anisaidie kuisimamia ikibidi kutafuta soko zuri .
Naomba mtu mwenye uwezo wa kuendesha hii biashara anisaidie kuisimamia ikibidi kutafuta soko zuri .