Msaada: Wapi zinauzwa chain saw?

Msaada: Wapi zinauzwa chain saw?

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Habari zenu wadau wa biashara,

Ninataka kununua chain saw kwa ajili ya kukatia miti kwenye shamba langu jipya ili kusafisha shamba kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kilimo.

sihitaji kubwa sana kama ya kupasulia mbao bali kukatia miti tu. Ila nataka iwe nzuri ili itumike kwa miaka kadhaa hata kwa shughuli nyingine za kukata miti n.k

Nimewahi kuiona mashine moja ya STIHL original... niliipenda. nikipata kama ile nitafurahi sana.

NB: sihitaji brand za china na india kama mashine za TOYO na nyingine za namna hiyo.

Nawategemeeni sana wadau.... naihitaji kwa haraka ili kazi ianze kabla msimu wa mvua haujaanza mikoa ya magharibi.
 
Location yako ipo Kigoma.
Kwa mkoa huo niliosoma mie,Nenda SIDO,nahisi bado wako ile njia ya kwenda Mlole Secondary.
Panda daladala za Kwenda Gungu au Mwandiga,mwambie Utingo naelekea SIDO atakuambia pa kushuka.

SIDO watan brands nyingi kwenye links zao,wanaweza kukuelekeza wapi na maduka gani mazuri ya kununua kifaa hicho.

Wengine watakuja kukupa maduka ya moja kwa moja,ila lazima iwe na DAR ila kwa mkoa huo huna option zaidi ya SIDO
 
Sido hawana mashine hizi hapa Kigoma.... nimetembelea madukani nimekuta za Toyo na zingine brand za kichina. Pia nimekuta HANSGAVNER kubwa yenye bei ghali sana. Pia ni kubwa sana kwa kazi nayotaka kuifanya.
 
Hiyo ndo best chain saw tena iwe 272 made in Brazil kwa dar ni 1.2mil
 
Hiyo ndo best chain saw tena iwe 272 made in Brazil kwa dar ni 1.2mil

Uko sahihi kaka..... ila kwa kusafishia shamba tu nadhani ni kubwa mno. Ingekuwa naenda kupasulia mbao. That would be my first choice!! Pia nalazimika kutafuta ya bei ndogo ili pesa nyingine niielekeze kwenye kuanza kazi. Nashukuru kwa mchango wako ndugu.
 
Ni kama nimeziona Kariakoo. Nenda utapata.
 
Uko sahihi kaka..... ila kwa kusafishia shamba tu nadhani ni kubwa mno. Ingekuwa naenda kupasulia mbao. That would be my first choice!! Pia nalazimika kutafuta ya bei ndogo ili pesa nyingine niielekeze kwenye kuanza kazi. Nashukuru kwa mchango wako ndugu.

Ungekuwa umejipanga bora ungenunua hii maana baada ya Kazi za shambani kwako ingetumika kama kitega uchumi
 
Hii biashara ya chain saw inalipa kiasi gani wakuu?

Isijekua ni fursa nzuri wengine hatuna habari
 
Keko Mwanga Dar mkabala na TEMESA ziko za aina mbalimbalil kwa bei nzuri.
Mimi si dalali wala si muuzaji ila ukitaka nitakudirect.
Kuna mzee huwa ananunua hapo mara nyingi.
 
Back
Top Bottom