Jamani tuache story, kama ni kweli huyu mtu anahitaji msaada wa ushauri ili kumweka katika hali nzuri kisaikolojia kwanza, ili aone kuwa na mimba ni changamoto tuu za maisha, na bado atafaulu masomo yake. Mimi nimesoma chuo na ninafahamu mifano mingi ya watu wa aina hiyo na wakishauriwa vizuri atatoka fresh tuu.
Jambo la pili ni msaada wa kifedha (ada). Mleta mada hajaweka hoja vizuri, kwani anapata % ngapi ya HESLB? na yeye atahitaji kutoa ngapi? Alafu watu wa karibu (marafiki, ndugu, wanaotoka naye sehemu moja, wilaya au mkoa, wanaosali naye, class mates wake, etc) wameshindwa kabisa kutoa suluhu ya tatizo hilo? Katika hali ya kawaida siamini katika hilo.
Naomba mtoa mada aweke wazi huyo dada yuko chuo gani, alafu wadau tutatoa ushauri afuate steps zipi ili kumsaidia. Mimi niko chuo kikuu kimoja (sitakitaja) lakini ninaweza kutoa ushauri nini kifanyike katika mazingira hayo. Nasema hivyo kwa sababu kuna ofisi ya dean of student ambayo kazi yake moja kubwa ni kumshauri mwanafunzi katika matatizo, pia kuna academic adviser ambaye ni Lecturer, ambaye pia anamshauri mwanafunzi katika matatizo ya kitaaluma. Pia Kuna social groups kwa mfano wanaotoka mkoa fulani wanakuwa na assocition yao kwa ajili ya kusaidiana mambo kadha wa kadha. Pia kuna vikundi vya dini, anaweza kupata ushauri na kuombewa pia kumtia moyo na kumwomba Mungu afungue njia kwa ajili yake. Mwisho wa siku solution itapatikana tuu hata kama ni kuchangishana vijisenti kidogo miongoni mwa hivyo vikundi na wasamaria mwema na ada itapatikana.
Kama kweli uko serious, naomba mleta mada ni PM kwa mawasiliano zaidi.