Msaada wapendwa nina gpa 2.8 accountancy

Msaada wapendwa nina gpa 2.8 accountancy

Tuntufye01

Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
19
Reaction score
10
Eti nitapata chuo kweli? Kila nikiingia kwny profile naona hivi
1475769797530.png
 
Subiri wanafanya udahili kama vigezo walivyoviweka unavyo utachaguliwa tu
 
hvi jukumu la gpa lipo nacte ama tcu mana naona waliochaguliwa hamna aliye chini ya gpa ya 3
 
udahili wa diploma kwenda degree tunaanza kuchukua GPA ya 3.0 na kuendelea wewe imekula kwako asante kwa ushiriki wako.
 
Gpa ni 3 kuendelea mwaka huu hapo umetoa sadak tu
 
jaribu kurisit mkuu upate gpa japo gentleman gpa kama ya baba riz
 
yani diploma uliapa utokuja kurisiti upate tu c-3 sasa ukatoka spidi tuna kupongeza ukamaliza lakini ajira ikawa bado kitendawili wazaz waka kushauri ukasome shahada sasa ndo yamekufikia hapo ushaur kuna maisha baada ya chuo fanya ishu nyingine kwa sasa utasota ingekuwa kipindi cha anko jk ahaaaa mapema tu ata huku jf usingekuja kabisa mana utachoshwa na comment za watu.....
 
Bora hiyo gpa ya 2.8 lakini unaimiliki kihalali kuliko yule mwenye 4.5 ya kuazima.
Kaambiwa lete original certificate, kaingia mitini.
 
Kama udsm diploma waliochukuliwa ni GPA ZA 4 + je wewe 2.8 yako nenda vile vyuo sijui zayon, sijui nn hua viko gorofani halafu chini kuna maduka
 
Back
Top Bottom