kimpango
JF-Expert Member
- Apr 24, 2011
- 600
- 717
Wadau nina ndugu yangu ambaye amefiwa na mkewe baada ya miaka minne ya ndoa yao ya kikristo.wote walikuwa ni wafanyakazi wa serikali kabla na baada ya kuoana.walipooana ndugu huyu alikuta marehemu mkewe akimiliki kiwanja maeneo flani jijini alichopewa na wazazi wake(alitoka kwenye familia ambayo watoto wote wamepewa viwanja vyenye hati ya majina yao ) Ndugu yangu pia alikuwa anamiliki viwanja vitatu lakini waliamua kuviuza viwili wakishirikiana na mkewe ili wapate hela ya kuyanza ujenzi,na baadaye waliamua kukopa kazini na kwa busara walikopa kutumia mshahara wa ndugu yangu wakajenga nyumba ikakamilika(deni bado lipo).(ndugu wote wanatambua hili)
Sehemu walipojenga ni karibu na nyumba na viwanja vya mashemeji wawili (nyumba yao ni kubwa) ,marehemu kabla hajaolewa na ndugu yangu alizaa mtoto mmoja wa kiume ambaye anaishi na baba yake nje ya nchi ,pia alizaa mtoto mwingine wa kike na ndugu yangu.
tatizo limeanza kwenye kikao cha uteuzi wa msimamizi wa mirathi ambapo ndugu yangu pamoja na kaka wa marehemu wameteuliwa kuwa wasimamizi lakini mali ikaamuliwa kuwa ni ya watoto,pia ndugu yangu amepewa sharti kuwa akae kwenye nyumba hiyo ila akitaka kuoa akapangishe au kujenga nyumba nyingine kwa hoja kwamba mke mpya anaweza kutesa watoto kwenye nyumba ambayo mama yao ameshiriki kuijenga
.
Msaada je nini haki ya mume(mgane) kwenye hali hii ....je maamuzi haya hayaweki hali ya nguvu yake kupotea vitu vyote vilivyonunuliwa kwa ujenzi wa nyumba vina jina la ndugu yangu kwenye risiti. Yeye hana tatizo na umiliki wa pamoja lakini kwake yeye anaona akikosa hela ya kujenga tena au kupanga asioe tena au pia kuoa ni kujitenganisha na mali walizochuma na marehemu mke wake. Wanasheria mtupe muongozo sahihi..nisameheni kuwachosha
nb ..bado hawajaenda mahakamani muhtasari ndio unaandaliwa ukiwa na hayo masharti