Latwifa Nkingwa
Member
- Mar 27, 2019
- 40
- 32
SHULE YA SEKONDARI MAURICE inawatangazia wazazi na walezi wote kwamba tunapokea wanafunzi kidato cha kwanza mwaka 2019, nafasi za kuamia kidato cha kwanza na cha pili pia tuna kituo cha mitihani kwa watahiniwa wa kujitegemea na Q.T. Vile vile pia tunapokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa michepuo ya ECA, HGE, HGK, HKL na HGL. ADA ni nafuu sana. Shule ni ya kutwa na bweni kwa wavulana na wasichana. Shule ipo Dar es salaam wilaya ya temeke, eneo LA mbande kisewe. Simu 0785907371. Wote munakaribishwa.Hivi mwaka huu wa 2019 kunavigezo gani vya kuchukua wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza? Maana Nina kijana wangu ana D3 na C1 na B moja na jina lake halikutoka sasa hivi wanadai anadaiwa akachukue form kwani amechelewa sana na Toto lenyewe hata shule halitaki
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakuu nimeomba msaada wa kufahamishwa kwa mwaka huu wa 2019 wanautaratibu gani?
ha ha ha haLianzishie Bishara ya Ice cream likatembeze mtaani
Siyakudumisa Nkosi Yezulu
Jibu langu jamani tafadhalini!Usipomsomesha huyo mtoto angalau akapata hata iyoo four ya 50 ,utakuwa umejitengenezea mwenyew bomu likilipuka hutaamin
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu huyu mtoto ukweli kabisa nimenyoosha mikono. Maana toka darasa la tano alianza Tabia ambazo ni za kutoroka nyumbani hadi wiki.Pengine zaidi na humu ndani Nina RB za kumtafuta ndani ya droo ziko karibu ishiriniKuhusu ufaulu sina hakika,nakushauri uende kwenye hiyo shule husika utapata majibu.
Kuhusu ukorofi wa mtoto wako,usiuchukie hiyo inatokana na mabadiliko katika ukuaji ni wewe tu kumrekebisha.Usipomsomesha ni sawa na kujiongezea au kutengeneza tatizo huko mbeleni.
Kama unaishi na mama yake mzazi hilo ni tatizo dogo, jaribuni kujadili pamoja na kuangalia wapi mlikosea kwenye malezi,rekebisheni.Mtoto wenu atakuwa alijiunga kwenye makundi ya wahuni na kutokana na hali hiyo madawa ya kulevya yako mwilini mwake na yamemuathiri ndio maana anatafuta ela kwa kila njia aweze kununua hizo bangi.Kama mzazi hutakiwi kumkana mtoto,unachotakiwa kwa sasa ni kutafuta kila njia mtoto wenu arudi katika hali yake.Vinginevyo watu watakuwa wanakupa ushauri wa ajabu ajabu huku katika nafsi zao wakijua wewe kuna sehemu uliteleza.Ndugu huyu mtoto ukweli kabisa nimenyoosha mikono. Maana toka darasa la tano alianza Tabia ambazo ni za kutoroka nyumbani hadi wiki.Pengine zaidi na humu ndani Nina RB za kumtafuta ndani ya droo ziko karibu ishirini
Na mbaya zaidi nimekuja kugundua ameanza na kuvuta bangi Na sijui anazitoa wapi kingine kawa mwizi kiasi kwamba hadi inaperekea jirani kunichukia
Maana linapoiba huko wanakuja nyumbani ni nawaambia jamani nyie mkamateni Pelekeni polisi ili afungwe.
Hivi kwa sasa hayupo hapa nyumbani karibu wiki2 na kaondoka kaniibia betri ya gari yangu akaenda kuuza nilipomwambia kalilete ulikolipeleka ndio sikumuona Tena.
Ikanilazimu ninunue betri nyingine mpya pasipokutegemea
Maana gari hii auto muda wote lazima uwake kwa betri.
Sasa ndugu zangu kunamsomi hapo? Tuongee ule ukwelituu!
Sent using Jamii Forums mobile app